Ijumaa, Oktoba 18, 2013

AJABU YA TAMBWE WA SIMBA, KILA JUMANNE HUUMWA

KILA ifikapo Jumanne au Jumatano ya kila wiki, mshambuliaji Mrundi wa Simba, Amissi Tambwe, anaugua.
Tambwe amekuwa akilalamika kuumwa kila siku hizo mbili zinapofika na gazeti hili limefuatilia kwa wiki tatu sasa.
Uchunguzi uliofanywa na Championi Ijumaa umebaini kuwa, wiki tatu zilizopita aliugua tumbo, wiki iliyofuata akawa wanasumbuliwa na malaria na juzi akawa anadai kusumbuliwa na malaria tena.
Akizungumzia hali hiyo, Tambwe alisema kuwa anahisi hiyo inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayotofautiana na kwao Burundi.
“Suala la siku labda limetokea tu lakini nimekuwa nikiugua kila wiki kutokana na kubadili mazingira ya hali ya hewa ya hapa nchini ambayo ninaona haijanipenda. Jana (juzi) niliugua tena malaria, lakini nashukuru ninaendelea vizuri hivi sasa na mechi ya Yanga nitacheza,” alisema Tambwe.
Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Simba akitokea Vital’O, ndiye nahodha wa timu ya taifa ya Burundi na sasa anaongoza kwa upachikaji mabao Ligi Kuu Bara, anayo nane.

0 comments:

Chapisha Maoni