Jumatano, Oktoba 16, 2013

AFRIKA YA KUSINI KULIPA FIDIA YA MAUAJI MGODI WA MARIKANA

Serikali ya Afrika Kusini imetakiwa kuzilipa fidia familia za wahanga wa mauaji ya mgodi wa Marikana nchini humo.

Mahakama Kuu ya Afrika Kusini imeitaka serikali ya nchi hiyo kutenga bajeti maalumu ili kuzilipa fidia familia za wachimba migodi wa wa mgodi wa Marikana ambao walipoteza maisha yao mwaka jana.
Hukumu hiyo imetolewa baada ya mawakili wa familia za wahanga wa wachimba migodi pamoja na wachimba migodi waliojeruhiwa kushinda kesi waliokuwa wamewasilisha mahakamani dhidi ya serikali ya Afrika Kusini wakitaka wateja wao walipwe fidia.
Katika mapigano ya Agosti 16 mwaka jana baina ya polisi na wachimba migodi waliokuwa katika mgomo huko Marikana watu wasiopungua 34 waliuawa, 78 kujeruhiwa na wengine 206 kutiwa mbaroni.

0 comments:

Chapisha Maoni