TASWIRA ya kimataifa ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye katika
siku za hivi karibuni aliibua mzozo wa kidiplomasia na Rais Jakaya
Kikwete, inaonekana kuchukua mwelekeo wa kuchuja badala ya kustawi kwa
namna ilivyokuwa miaka michache tu iliyopita.
Baada ya kuvuma kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, Kagame, aliyekuwa akibeba taswira ya mtu shupavu na shujaa, amegeuka na kuanza kuonekana kiongozi mpenda vita, makuu na rais anayeweza kusababisha kuibuka na kukua kwa ufa mkubwa wa kimahusiano kati yake binafsi na viongozi wenzake wa ukanda huu wa Afrika. Nje ya bara hili, kuzorota kwa taswira ya kiongozi huyo kunaonekana kuanza kugusa hisia za wachambuzi wa masuala ya kisiasa, wanadiplomasia wanaoheshimika na viongozi wakuu wa mataifa ya Ulaya, Marekani na ndani ya Umoja wa Mataifa.
Baada ya kuvuma kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, Kagame, aliyekuwa akibeba taswira ya mtu shupavu na shujaa, amegeuka na kuanza kuonekana kiongozi mpenda vita, makuu na rais anayeweza kusababisha kuibuka na kukua kwa ufa mkubwa wa kimahusiano kati yake binafsi na viongozi wenzake wa ukanda huu wa Afrika. Nje ya bara hili, kuzorota kwa taswira ya kiongozi huyo kunaonekana kuanza kugusa hisia za wachambuzi wa masuala ya kisiasa, wanadiplomasia wanaoheshimika na viongozi wakuu wa mataifa ya Ulaya, Marekani na ndani ya Umoja wa Mataifa.
Siku chache baada ya Rais
wa Marekani, Barack Obama, kukaririwa na vyombo vya habari mbalimbali
duniani akimtaka Rais Kagame kuacha kukisaidia kijeshi kikundi cha waasi
wa M23, kidole hicho cha lawama kinaonekana kuungwa mkono kwa kasi na
makundi mengine ya kimataifa.
Kagame, ambaye kwa miaka mingi
amekuwa kiongozi kipenzi cha mataifa ya Ulaya na hasa Marekani tangu
alipofanikiwa kumaliza mapigano yaliyosababisha mauaji ya halaiki nchini
kwake mwaka 1994, katika siku za hivi karibuni taswira yake inaonekana
kubadilika na kuchukua mwelekeo wa lawama zaidi kuliko sifa.
Matamko
na maandishi yenye mwelekeo wa lawama ambayo yalitolewa dhidi yake
katika siku za hivi karibuni yameanza kuchukua mwelekeo unaoonyesha
kwamba Kagame wa sasa si yule tena aliyekuwa akitajwa kuwa mfano wa
kuigwa wa viongozi wapenda maendeleo na wazalendo wa kweli katika
Afrika.
Tukio la hivi karibuni kabisa, ni makala ya uchambuzi
iliyochapishwa katika gazeti la Uingereza la The Telegraph, ambayo
ilieleza namna majeshi ya Rwanda yalivyokuwa yakijipenyeza ndani ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kutoa misaada ya silaha na
vyakula kwa kundi la waasi wa M23, ambalo limekuwa likipigana Mashariki
mwa nchi hiyo tangu mwaka 2010.
The Telegraph katika makala yake
hiyo lilidurusu ripoti ya Shirika la Kimataifa la kutetea haki za
binadamu la Human Right Watch, iliyotolewa mwezi mmoja uliopita, ambayo
pamoja na mambo mengine, iliainisha ushahidi wa namna vikosi vya Jeshi
la Rwanda vilivyokuwa vikishiriki katika vitendo vya kiharamia ndani ya
DRC.
Katika uchambuzi wa ripoti hiyo, The Telegraph limeainisha kwamba ndani ya Rwanda, wanaume na vijana wadogo wenye umri wa miaka 15 wamekuwa wakilazimishwa kupewa mafunzo ya kupigana kijeshi kwa lengo la kulinda maeneo yenye utajiri wa madini katika mpaka wa nchi hizo mbili.
Katika uchambuzi wa ripoti hiyo, The Telegraph limeainisha kwamba ndani ya Rwanda, wanaume na vijana wadogo wenye umri wa miaka 15 wamekuwa wakilazimishwa kupewa mafunzo ya kupigana kijeshi kwa lengo la kulinda maeneo yenye utajiri wa madini katika mpaka wa nchi hizo mbili.
The
Telegraph limeandika kuwa licha ya utetezi wa awali wa Uingereza juu ya
misaada inayopelekwa Rwanda kuwa haimaanishi nchi hiyo inakwenda vitani
Kongo, lakini sasa uhalisia wa tuhuma dhidi Rwanda umejiweka hadharani.
Andrew
Mitchell, Katibu wa zamani wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa nchini
Uingereza, alikuwa mstari wa mbele wa kumtetea Rais Kagame dhidi ya
shutuma za kuchochea mapigano Kongo, pamoja na kupingwa vikali na mbunge
wa nchi hiyo, lakini Julai mwaka jana alifanikiwa kuidhinisha msaada wa
pauni milioni 16 kwa ajili ya serikali ya Rwanda.
Awali Mitchell
alipata kumshawishi Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, kwamba
madai yaliyokuwa yakiihusisha serikali ya Kagame na tuhuma za kuwaunga
mkono waasi wa M23 hayakuwa na ukweli.
Ushawishi huo ambao
ulipingwa vikali na wabunge wa nchi hiyo katika mjadala wa bajeti ya
misaada, hatimaye ilisababisha Mitchell alazimike kung’atuka katika
nafasi hiyo ya uongozi kwa sababu za kisera.
Kitendo cha wabunge
kupinga mtazamo huo wa Mitchell kutokana na kuwa na imani yao kwamba
Rwanda imekuwa ikisaidia kundi la waasi wa M23, mrithi wa kiti chake,
Justice Greening, alilazimika kufuta misaada ya kifedha kwa taifa hilo
yenye thamani ya jumla ya pauni milioni 21 mwishoni mwa Novemba, mwaka
jana.
Mwanzoni mwa mwaka huu, Kagame alipata kukaririwa akieleza
namna alivyokuwa akikerwa na maamuzi ya Jumuiya ya Kimataifa kuikatia
misaada Rwanda, hatua alizozielezea kwamba zitalifanya taifa hilo
liendelee kustawi.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, ndani ya Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa, ziliibuka tuhuma zilizoelekezwa kwa
Kagame na Majeshi ya Rwanda kwa namna walivyokuwa wakishiriki katika
mapigano ndani ya DRC.
Alikuwa ni Balozi wa Kudumu wa Ufaransa
ndani ya baraza hilo, Alexis Lameck, ambaye alikariri taarifa za kutoka
kwa Msemaji wa UN aliyeko Kinshasa nchini Kongo, Edmond Mulet, ambazo
zilikuwa zikiinyooshea Rwanda kidole cha namna ilivyokuwa ikishirikiana
na M23.
Shutuma mpya dhidi ya Kagame zinakuja ikiwa ni takribani
mwezi mmoja sasa, tangu gazeti hili la MTANZANIA Jumapili lilipoandika
kwa mara ya kwanza namna taswira ya sasa ya kiongozi huyo inavyoweza
kuwa mwanzo wa hatma mbaya kwake.
Katika gazeti hilo, ilielezwa
namna Kagame anavyokabiliwa na hatari ya kufikishwa mbele ya Mahakama ya
Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), kama ilivyopata kuwa kwa aliyekuwa
Rais wa Liberia, Charles Taylor.
Kama ilivyo kwa Kagame
anavyohusishwa na vita ya Kongo, Taylor alituhumiwa kwa miaka mingi kama
mbabe wa vita vya Sierra Leone, ambayo iligharimu maisha ya takribani
zaidi ya watu 50,000.
Kwa sasa Taylor anatumikia kifungo cha miaka 50 jela, baada ya kupatikana na makosa ya uhalifu wa kivita nchini Sierra Leone.
0 comments:
Chapisha Maoni