WILAYA
YA MBEYA MJINI - MAUAJI.
MNAMO TAREHE 08.09.2013 MAJIRA YA SAA
14:15HRS HUKO KATIKA HOSPITALI
YA RUFAA MBEYA JIJI NA MKOA WA
MBEYA. MUSA
MBUKWA, MIAKA 30,
MFIPA, MKULIMA, MKAZI WA NSALAGA – UYOLE ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA
KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO BAADA YA
KUJERUHIWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI TAREHE 08.09.2013 SAA
10:00HRS KWA TUHUMA ZA WIZI WA
BAISKELI AINA YA BAMBUCHA YENYE THAMANI
YA TSHS 125,000/= MALI YA CHRISTOPHER MWAITEGE, MIAKA 39,
MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA GOMBE. MBINU
NI KUMSHAMBULIA MAREHEMU KWA KUTUMIA
SILAHA ZA JADI MAWE NA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE WAKATI AKIWA
NJIANI ANAPELEKWA KITUO CHA POLISI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALINI HAPO. JITIHADA ZA KUWABAINI NA KUWAKAMATA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI
ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA BADALA YAKE WAWAFIKISHE KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA
WANOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
Imesainiwa
na:
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Chapisha Maoni