WILAYA YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA
PIKIPIKI NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 06.09.2013 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO ISYONJE BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA
WA MBEYA. GARI NO T.906 AJK T/HIACE LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA MPANDA PIKIPIKI NO T.215 CMM BOXER ILIYOKUWA
IKIENDESHWA NA EMMANUEL S/O MGIMWA,
MIAKA 59, MHEHE, AFISA KILIMO WA IDWELI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.
CHANZO CHA AJALI NI DEREVA WA HIACE KUTAKA KULIPITA GARI LA MBELE YAKE BILA
KUCHUKUA TAHADHARI. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO HILO JUHUDI ZA
KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO
VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA
KWA
MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 06.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:10HRS HUKO ISANGA BARABARA YA MBEYA/CHUNYA GARI NO. T.156 AHN SCANIA BUS LIKIENDESHWA NA DEREVA BARAKA S/O MGALULA, MIAKA 37, MSUKUMA
NA MKAZI WA TABORA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AITWAYE KANUNU S/O PENJA, MIAKA 75, MNYAKYUSA NA MKAZI WA ISANGA NA
KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed
by:
[DIWANI
ATHUMANI - ACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA
0 comments:
Chapisha Maoni