Mtangazaji nyota nchini ambae ni mchumba
wa kupika na kupakua wa mwanamuziki Diamond Penny amevunja ukimya na
kutoa onyo kali kwa wasanii wa kike na wasio wasanii kumlaia mbali baby
boy wake Diamond.
Habari za uhakika toka kwa mtu wa karibu
na Penny anaeishi nae maeneo ya Mwananyamala ambae pia aliomba hifadhi
ya jina lake alisema “ Jamani Penny amejipanga kuolewa na Diamond kwani
sasa hivi amecharuka na kutoa onyo kali kwa mwanamke yeyote atakae
msogelea mchumbaake huyo la sivyo ataroka mtu” Alisema dada huyo ambae
anafanyakazi nyumba ya jirani na anapoishi Penny
Penny amepiga mkwara huo hasa akimlenga
zaidi msanii Lulu na Linah nk huku akitahadharisha kuwa anawaomba wote
wenye tabia ya kuchukua wanaume za watu kwani yeye katika maisha yake
hajawahi kuchukua mume wa mtu hivyo kama akihisi kuna ajenda yoyote ya
siri kati ya mchumbaake na wasanii hao hakika ataroga mtu kwani yeye ni
mtoto Mdigo halisi.
Aidha chanzo hicho kiliongeza kusema
kuwa penzi la Penny na Diamond limefikia pazuri kiasi cha familia zao
kutembelea na kula pamoja kama wakwe. Hata hivyo ilielezwa kuwa Familia
ya Diamond imeshampa Baraka zote mtoto wao ili amuoe kabisa Penny na
huku nae Penny akihimizwa kudumisha upendo wa dhati kwa Diamond ambae
tangu aanze kuishi na mtangazaji huyo Diamond amebadilika sana kitabia
kiafya
0 comments:
Chapisha Maoni