Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye sasa ni mjasiriamali
pia Anasteria Sanga Linah au muite Ndege Mnana amefunguka kuwa producer wa
studio ya Bhitz Pancho Latino ndiye mwenye siri nzito ya penzi lake na msanii
mwenzake Amini ambaye kwasasa penzi lao limekuwa stori ya kale baada ya
kuachana.
Linah amesema tokea wanaanza mapenzi yao Pancho ndiye alikuwa mtu pekee
anayejua mambo mengi kuwahusu wao na jinsi walivyotumbukia katika penzi ambalo
anasema yeye binafsi ndiye hasa alikuwa akimpenda Amini kupita kiasi japo
baadaye akagundua kuwa hata mwenzake naye anamzimika na hivyo penzi likawa
linasonga.
"Yaani we muulize Pancho yule ndio ana siri kubwa sana ya penzi langu na
Amini,yaani jamani nilimpenda sana Amini mpaka nikakubali kuingia kwenye
mapenzi na nilimpenda hasa kutoka moyoni,kuna vitu vingi nyuma yake ambavyo
Pancho anajua",alisema Linah.
Msanii huyo mwenye sauti tamu kiasi cha kupachikwa jina la Ndege Mnana na
msanii mkongwe Patricia Hillary ameendelea kufunguka kuwa wakati ameangukia
katika penzi la Amini alikuwa anawachomolea wanaume wengi waliokuwa wanamtokea
tena wenye pesa zao na wengine ni watu wazito lakini aliamua kutoka moyoni kwa
dhati kuwa na Amini kwahiyo akawa anamtunzia heshima yake.
Anasema kama angekuwa macho juu kuna uwezekano mkubwa asingeendelea kuwa na
Amini au angekuwa anamsaliti kwa kiasi kikubwa lakini moyo wake usio na tamaa
ndio ulikuwa unamfanya aendelee kumpatia penzi la kweli.
Akavujisha siri kuwa Amini ndiye aliyemtibua na ndipo akapitisha uamuzi wa
kujiweka pembeni kwasababu ambazo ni ngumu kuziweka hadharani lakini mpenzi
wake huyo wa zamani anazijua na ni sababu ambazo haziwezi tena kulirudisha
penzi lao japo anakiri kuwa aligundua kuwa mpenzi wake huyo wa zamani anampenda
siku alipomtamkia kuwa mapenzi yameisha kila mmoja ashike lake.
Anasema katika kuonesha kuwa ameachana na Amini lakini hana bifu naye wakaamua
kutoa wimbo wa pamoja wa Mtima wange.
Akizungumzia show anazofanya na Amini jukwaani wakiwa kama wapenzi anasema ni
kuonesha kuwa hakuna bifu na hata mabusu anayopigwa na zilipendwa wake huyo
anayapokea kwasababu anashindwa kuyapotezea jukwaani akiogopa kumtia aibu jamaa
huyo mbele ya mashabiki na watu wengine.
0 comments:
Chapisha Maoni