Jumapili, Septemba 08, 2013

BAHATI BUKUKU KUZINDUA DUNIA HAINA HURUMA BURE LEO

Rose Muhando, Christina Shusho, Bonny Mwaitege, Martha Mwaipaja, Upendo Nkone, Edson Mwasabwite, Jennifer Mgendi, Christina Matai, na wengineo wengi tu watakuwepo kumsindikiza Bahati Bukuku wakati wa tamasha la kuzindua DVD ya dunia haina huruma bure kabisa.
Katika mahojiano na Silas Mbise kupitia Gospel Celebration ya WAPO Radio FM, Bahati anaeleza sababu ya kufanya uzinduzi huo bure ni kwamba anahitaji watu wengi wafike kwenye ukumbi wa PTA kwenye viwanja vya sabasaba, kwa kuwa imekuwa desturi ya baadhi ya watu kutofika kutokana na kukosa hela ya kiingilio, sasa hapa anawaambia kuwa wajipange kwa nauli yao tu na kwenda siku hiyo (Jumapili tarehe 8) wapate kununua DVD yake kwa mara ya kwanza itakapoanza kuuzwa.
Kwa maelezo ya Bahati Bukuku, basi hauna sababu ya kukosa kuhudhuria kwenye tamasha hilo litakaloanza mishale ya saa 8 mchana na kuendelea.

0 comments:

Chapisha Maoni