Alhamisi, Agosti 08, 2013

MTOTO WA MIAKA 5 AFARIKI PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI MBEYA

Mtoto mmoja  amefariki baada kugongwa na pikipiki huko kijijini Ndaga, wilayani Rungwe mkoani ,Mbeya jana majira ya saa 11 jioni.
Taarifa toka makao makuu ya polisi mkoani Mbeya zinasema kuwa mtoto Willy Edward (5), Msafwa na mkazi wa kijiji cha Ndaga alipatwa na mauti papo hapo baada ya kugongwa na pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na Rashid Issa (32), Mkinga na mkazi wa kijiji cha Ntokela.
Aidha tukio hilo lililotukia majira ya saa 11 jioni lilihusisha pikipiki aina ya T-BETTER yenye namba za usajili T.101 CDR lilisababishwa na mwendo kasi. Dereva anashikiliwa na jeshi la polisi na taratibu zinaendelea ili afikishwe mahakamani.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Rungwe, pia kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya bw. Diwani Athuman ametoa wito kwa madereva kuwa makini watumiapo vyombo vya moto kwa kuzungatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali za mara kwa mara.

0 comments:

Chapisha Maoni