Polisi nchini Musumbiji wameonya
kuwa wamaume wenye vipara huenda wakalengwa kwenye mashambulizi
yanayohusiana na uchawi, pamoja na matambiko fulani, baada ya kuuliwa
kwa wanaume wawili kama hao mwezi uliopita.
Wanaume hao wawili
wenye upara na ambapo mmoja wao alipatikana akiwa amekatwa kichwa na
viungo vya mwili vikiwa vimetolewa, waliuliwa katika mkoa wa Zambezi.
"Mwezi
uliopita mauaji ya watu wawili wenye vipara yalisababisha kukamatwa kwa
washukiwa wawili," msemaji wa polisi Inacio Dina, alisema kwenye
mkutano wa waandishi wa habari mjini Maputo.
Mwenyeji mjini Maputo anasema kuwa baadhi ya watu wana
imani potovu kuwa watu wenye vipara wako na dhahabu kwenye vichwa vyao.
Visa vya kuuliwa watu wenye upara kwa maswala ya uchawi havijaripotiwa siku za nyuma.
Washukiwa
ni vijana wa Msumbiji, waliowaambia polisi kuwa viungo hivyo
vingetumiwa kwa uchawi na matambiko nchini Tanzania na Malawi.
Tanzania inafahamika duniani kwa watu wenye matatizo ya ngozi kuuwawa na viungo vyao kutumika kwenye matambiko ya kichawi.
0 comments:
Chapisha Maoni