MREMBO wa filamu nchini, Wastara Juma, amesema marehemu Steven Kanumba alikuwa mshenga wa marehemu mume wake, Juma Sajuki.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Wastara alisema wengi
wamekuwa hawajui historia yake na kusema baada ya yeye kupata ajali,
alimlazimisha Sajuki kumuoa kitu ambacho sio kweli.
Usilolijua ni kama usiku wa giza, Sajuki ndie alifanya haraka kunioa baada ya kupata ajali, na mshenga wake alikuwa Kanumba, hivyo mimi sikumlazimisha Sajuki kunioa, naomba jamii ielewe hivyo
alisema
Wastara kwa uchungu.
Aidha, alisema kwa kukutana na changamoto nyingi katika kazi zake, ameamua kutafuata meneja ambaye wanatasaidiana.
Tangu nimefiwa filamu ambazo nimefanya mwenyewe ni kama mbili tu, changamoto zilizopo kwangu, ninafanya kazi peke yangu kazi zinakuwa nyingi na sina msaada.Nimeamua kumtafuta meneja ambaye atanisaidia baadhi ya kazi muhimu kwa sababu watu wanahitaji kazi nzuri, kwa hali hiyo imenilazimu nitafute mtu wa kusaidiana nae
alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni