Siku kama ya leo miaka 101 iliyopita Profesa Roger Garaudy, mwanafalsafa
na mwanafikra wa Ufaransa alizaliwa huko katika mji wa Marseille.
Garaudy alipata shahada ya daraja ya udaktari katika taaluma tatu za
masomo ya falsafa, fasihi na utamaduni. Roger Garaudy alifungwa jela
katika kambi ya mateka wa kivita wa Ujerumani tangu mwaka 1940 hadi 1943
kutokana na mapambano yake dhidi ya ufashisti wa Adolph Hitler wakati
Ufaransa ilipokaliwa kwa mabavu na Ujerumani. Profesa Garaudy alikuwa
mwanachama wa chama cha Kikomonisti cha Ufaransa kwa miaka 36 na pia
mwanachama wa kamati kuu ya chama hicho kwa miaka 25. Hata hivyo
mitazamo ya kikomunisti na kiliberali haikuweza kukata kiu ya kutafuta
ukweli ya msomi huyo wa Ufaransa na hatimaye alikubali dini ya tukufu ya
Kiislamu baada ya kufanya utafiti mkubwa. Ushindi wa Mapinduzi ya
Kiislamu nchini Iran mwaka 1979 ulikuwa na taathira kubwa katika
mitazamo ya Profesa Roger Garaudy.
Na miaka 46 iliyopita katika siku inayosadifiana na hii ya leo chama cha Baath cha Iraq kilichukua hatamu za uongozi kupitia mapinduzi yaliyoongozwa na Ahmad Hassan al Bakr na kumpindua Rais Abdulrahman Aarif. Baada ya kuchukua madaraka chama cha Baath, Saddam Hussein ambaye alikuwa kiongozi nambari mbili wa chama hicho alianza kuwauwa wapinzani wake nchini Iraq na vikosi vya usalama na vya jeshi la nchi hiyo pia vikaanzisha hujuma kali dhidi ya Wakurdi wapinzani, wazalendo, wanaharakati wa Kiislamu na hata Wakomonisti.

0 comments:
Chapisha Maoni