Agnes Marwa (18), mkazi wa Mrito, Kata ya Kemambo, Wilaya ya
Tarime, mkoani Mara, ameunguzwa sehemu za siri kwa moto baada ya mume
wake kudaiwa kumkuta na Sh2,000 kwenye pochi.
Inadaiwa baada ya kumkuta na fedha hizo,
alimtuhumu kuhongwa na wanaume na kuanza kumpiga, kisha kumfunga nje
akinyeshewa na mvua baadaye kuchukua kiginga cha moto na kumchoma sehemu
za siri.
Akisimlia mkasa huo kwenye Kituo cha Afya
Sungusungu Nyamongo alikolazwa, Agnes alisema mumewe amekuwa na tabia ya
kumpiga hivyo aliona ni hali ya kawaida, lakini alishtuka baada ya
kupelekwa nje na kufungwa kwenye mti na kuanza kuchomwa moto.
Alisema alilia sana kuomba msaada kutokana na
maumivu aliyokuwa anayapata, lakini hakuna mtu wa karibu aliyejitokeza
kutokana na mumewe kuogopwa na majirani kwa ubabe wake.
0 comments:
Chapisha Maoni