Jumanne, Julai 22, 2014

MCHUNGAJI MWENYE WAKE 11 ABAKA WANAWAKE WANNE KANISANI KWAKE


Robert Martin Gumbura, mchungaji kutoka nchini Zimbabwe mwenye wake 11 amewabaka wasichana wanne ambao ni waumini wa kanisa lake nchini humo. 
Mchungaji Robert Martin Gumbura akiwa chini ya ulinzi
Mchungaji huyo ambaye ni mwanzilishi wa kanisa liitwalo‘Robert Martin Gumbura Independent End Time Message Church’ amehukumiwa kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka 50 siku ya jana jumanne kwa kosa la kuwabaka na kuwadhalilisha wanawake hao kijinsia.
Wake 11 wa mchungaji Robert Martin Gumbura
Taarifa zilizoifikia Fichuo Tz zinaeleza kuwa mchungaji huyo mwenye umri wa miaka 57 ambaye tayari anao wake 11 na watoto 30 alidai kwamba wanachama wote wa kike wa kanisa lake walikuwa na wake zake kwa haki, na wanawake walioolewa walikuwa wakiishi na  waume zao kimkopo kwa kuwa nao ni wake zake kihaki.
Hakimu katika mahakama iliyotoa hukumu hiyo, hakimu Hoseah Mujaya alisema,
Wewe ni mbwa mwitu uliyejivika ngozi ya kondoo. Kazi ya msingi ya kanisa lolote ni ibada na si kulala na wasichana na wanawake na waahidi kwamba endapo watakaa hilo basi balaa litawakumba.

0 comments:

Chapisha Maoni