Polisi wa Argentina wamepambana na waandamanaji katika mji mkuu, Buenos
Aires baada ya nchi hiyo kufungwa na Ujerumani katika mchezo wa fainali
ya Kombe la Dunia.
Mapema jana jioni maelfu ya watu walikusanyika katika mnara wa Obelisk jijini humo ili kusherekea licha ya kupoteza mchezo huo.
Hata hivyo, baadaye usiku, hali ilibadilika na vijana kuanza kuwarushia
polisi mawe na kuvunja maduka. Watu wasiopungua 50 walikamatwa huku
polisi 15 wakijeruhiwa.
Mapema jana jioni maelfu ya watu walikusanyika katika mnara wa Obelisk jijini humo ili kusherekea licha ya kupoteza mchezo huo.
0 comments:
Chapisha Maoni