Kwa mujibu wa rafiki wa
karibu wa mkali huyo wa sinema za Kibongo, hata mashosti zake hawajui
kinachoendelea zaidi ya kuulizana wao kwa wao kuhusu nini kinaendelea
huku kukiwa na hisia kuwa huenda wawili hao wamefunga ndoa ya siri.
Kuna maelezo kwamba Diamond alifanya hivyo ili kuzuia mwanaume mwingine kumvisha Wema pete ya ndoa kwani alishamvisha ya uchumba tangu mwaka 2011 kwenye Ukumbi wa New Maisha ulipo Masaki jijini Dar.
Kuna maelezo kwamba Diamond alifanya hivyo ili kuzuia mwanaume mwingine kumvisha Wema pete ya ndoa kwani alishamvisha ya uchumba tangu mwaka 2011 kwenye Ukumbi wa New Maisha ulipo Masaki jijini Dar.
Wiki iliyopita jitihada za kumnasa Wema akiwa na pete ya uchumba zilizaa matunda ambapo mwanahabari wetu alimuweka ‘mtukati.
Wema alipotakiwa kuanika ukweli juu ya pete hiyo, alikubali na kueleza
kuwa ameamua kufunguka kwa mwanahabari wetu baada ya kuwa kimya tangu
alipovishwa pete hiyo.
Wema alisema si kweli kwamba amefunga ndoa
ya siri ila Diamond alimvisha pete hiyo kama urembo akijua kabisa kwamba
yeye ni wife material (anafaa kuwa mke).
Sijafunga ndoa jamani. Hii pete alininunulia baby wangu Nasibu (Diamond) wakati tukiwa South Africa (Afrika Kusini).
Alininunulia na kunivisha tulipokwenda kwenye Tuzo za MTV Africa (MAMA). Nakumbuka tuliingia kwenye duka moja nikaiona hii pete ikanivutia sana, nikamwambia Nasibu ndipo akaninunulia na kunivisha palepale.Cha kushangaza ni kwamba imewatatiza wengi na kuhisi ndoa tayari.
Hii pete ndogo niliinunua mwenyewe hapahapa Bongo na kuivaa kama urembo tu, hakuna tofauti na hilo kuhusiana na hizi pete nilizovaa kidole husika
alisema Wema ambaye kidoleni kwake kunaonekana pete
mbili, kubwa na ndogo.
(kicheko) hilo sina uhakika nalo but amegundua mimi ni wife material hataki kunipoteza. Kanipa heshima anayostahili kupewa mwanamke...
Wakati huohuo, Wema
amemshukuru mtabiri, Maalim Hassan Yahya ambaye mwanzoni mwa mwaka huu
alitabiri kuwa mastaa hao wataoana mwezi ujao (Agosti) mwaka huu akiomba
Mungu na iwe hivyo.
Natamani hiyo ndoa na nasubiria hiyo siku ili utabiri utimie, ni jambo la heri jamani
alisema Wema.
Alipotafutwa Diamond ili afunguke
kuhusiana na ishu hiyo, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
Wakati huohuo, mashabiki wa mastaa hao, wamewashauri mama Wema na mama
Diamond kuwa kitu kimoja ili kufanikisha ndoa hiyo ya watoto wao.
Ukiacha pete hiyo ya
ndoa aliyovishwa na Diamond, Wema aliwahi kuvishwa pete kama hiyo
alipofunga ndoa na jamaa aitwaye Jumbe Yusuf Jumbe ambayo haikudumu hata
mwezi mmoja.
0 comments:
Chapisha Maoni