Mtu mmoja aliye julikana kwa majina Fedelisi Muhamedi (40) mkazi wa
kijiji cha Malolo mikumi mkoani Morogoro anashikiliwa na jeshi la polisi
kwa tuhuma za kukutwa na meno manne ya tembo baada ya kuuwa tembo
wawili.
Kamamda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema mnamo
tarehe 22 june majira ya saa 12 jioni katika kijiji cha Malolo mikumi
kwenye hifadhi ya udizungwa wananchi walisikia mlio wa risasi ambapo
tayari tembo wawili madume waliuawa na kutolewa meno ambapo wananchi
walitoa taarifa kwa jeshi la polisi na jeshi hilo kuanza msako na
kumkamata mtuhumiwa Fedelisi Muhamedi aliyewaonyesha sehemu
yalikowekwa meno hayo yakiwa pamoja na bunduki moja na shoka vifaa
wanavyotumia kuwaulia tembo.
Aidha kamanda Leonard Paul amewataka wananchi mkoani Morogoro
kushirikiana na jeshi la polisi kubani na kutoa taarifa za uhalifu
katika maeneo yao ili yaweze kudhibitiwa mara moja huku akiwataka
wananchi kusherekea sikukuu ya Edd il fitri kwa amani na utulivu ambapo
amewahakikishia wakazi wa mkoa wa Morogoro jeshi litaimarisha ulizi
katika maeneo yote ya ibada katika kukabiliana na matukio ya uhalifu.
0 comments:
Chapisha Maoni