Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal anatarajia
shirikisho la soka duniani FIFA litawaruhusu wachezaji wake kunywa maji
katika mechi yao ya raundi ya pili dhidi ya Mexico itakayochezwa
katika uwanja wa Castelao ulioko katika eneo la Fortaleza.
Fortaleza ni eneo linaloshuhudia viwango vya juu vya nyuzi joto.
Kocha huyo wa Manchester United ya
Uingereza anasema kuwa utafiti uliofanywa kabla ya mashindano haya
yanasema kuwa wachezaji wanapoteza maji lita nne ama zaidi kwa kila
mechi wanayocheza katika jimbo hilo la Fortaleza.
Ni dhahiri kuwa mwili wa binadamu yeyote
unastahili maji kwa hivyo hawa wachezaji naamini kuwa wanastahili kunywa
maji ilikuzuia wasishikwe na kisunzi .
Van Gaal alitishia
kuwapa wachezaji wake maji kwa wingi kando kando mwa uwanja iwapo FIFA
haitahalalisha kuwepo kwa dakika moja au mbili ambapo mechi
zitasimamishwa iliwachezaji wake wapige kopo la maji.
Kiungo wao Leroy Fer, ambaye anauguza jeraha la
goti anasema kuwa Uholanzi ilipata kionjo tu cha kucheza katika hali ya
kiwango cha juu mno cha joto baada ya kuwasili huko wakitoka Rio de
Janeiro.
Fer anasema kuwa japo Uholanzi imezoea kucheza
katika maeneo ya Uropa yenye baridi kali,Uholanzi itajikaza kisabuni
kwani ni hali ileile itakayoikumba timu pinzani ya Mexico.
0 comments:
Chapisha Maoni