Kila mmoja ana uhuru na haki ya kupenda. Huwezi kuchaguliwa wa kumpenda! Mapenzi ni maisha ya mtu katika uhalisia wake.
Hii humaanisha kuwa kama utakuwa na mtu ambaye moyo wako hauna
mapendo ya dhati kwake, tafsiri yake ni kwamba, maisha yako yote
yatakuwa yenye mateso kila siku.
Utalala na mtu usiyempenda, utaamka naye na utaambatana naye baadhi
ya sehemu wakati moyo wako haukuwa tayari kuwa naye. Hilo ni tatizo. Kwa
bahati mbaya kuna baadhi ya wazazi bado wana mawazo na fikra za
kizamani.
Wapo wanaoendelea kuwachagulia au kuwalazimisha watoto wao wenzi wa
kuishi nao. Ndugu zangu, hizo ni zama za kale. Maisha yamebadilika. Kila
kitu kimebadilika. Ni sahihi zaidi mtu achague mwenzi wa maisha yake
mwenyewe maana ataishi naye yeye na siyo mzazi au mwingine yeyote.
Huo ni upande mmoja; upande mwingine ni haki ya mwanamke kupenda.
Imezoeleka mwanaume ndiye mwenye mamlaka ya kumpenda mwanamke na kumtaka
waanzishe uhusiano.
Inategemea kama mwanamke atakubali au atakataa. Pengine ni utaratibu
sahihi maana ni uamuzi wa mwanamke na kuangalia moyo wake kama ni kweli
amempenda mwanaume huyo au lah kisha anaamua mwenyewe.
Kuna wakati mwanamke anazama katika mapenzi kwa mwanaume. Kila
akipita mbele yake, moyo unalipuka. Kila anachokifanya anazuzuka.
Mapenzi yamemwingia lakini sheria inambana. Hawezi kuanzisha uhusiano
yeye.
Hata kama akiamua kujipeleka, mwisho wao hauwi mzuri – wataachana tu
(mara nyingi). Tafiti zinaonyesha kuwa, uhusiano ulioanzishwa na
mwanamke mara nyingi huwa hauna mafanikio kama unaoanzishwa na mwanaume.
Akili za wanaume wengi huamini mwanamke anapomfuata na kumtaka
kimapenzi ni mhuni au kwa lugha za vijana anaonekana hajatulia! Si jambo
sahihi, hutegemea na moyo wa mhusika na namna anavyoonesha mapenzi yake
lakini ndivyo ilivyozoeleka.
Pamoja na hayo, mwanamke anaweza kumvutia mwanaume aliyempenda na
kumuingiza kwenye himaya yake kwa kufuata utaratibu ulio sahihi na penzi
likadumu.
Kwanza
utajihakikishia kuwa huonekani mhuni na bado uhusiano wenu ukawa wenye
nguvu, penzi la dhati na lenye kuvutia. Hakika inawezekana. Ni suala la
kufuata tu utaratibu uliopendekezwa.
Hapa chini sasa nitakupa mbinu rahisi ambazo zinaweza kukusaidia
kumnasa mwanaume anayeusumbua moyo wako. Kwa nini uteseke wakati njia za
kumnasa zipo? Hebu twende tukajifunze...
MVUTO
Kwanza kabisa, kama mwanamke unapaswa kuwa katika mwonekano mzuri wa kike wenye kuvutia muda wote. Hapa nasema hivyo kwa sababu wapo wanawake ambao wanahangaika na hawajaolewa au hawajapata watu waliotangaza nia kwa sababu tu hawajiweki katika mwonekano mzuri.
Kwanza kabisa, kama mwanamke unapaswa kuwa katika mwonekano mzuri wa kike wenye kuvutia muda wote. Hapa nasema hivyo kwa sababu wapo wanawake ambao wanahangaika na hawajaolewa au hawajapata watu waliotangaza nia kwa sababu tu hawajiweki katika mwonekano mzuri.
Mwanamke jitambue. Tengeneza na hifadhi mvuto wako siku zote. Zingatia mavazi bora, yenye staha na kukusitiri.
Baadhi ya wanawake huamini katika mavazi yanayowaacha baadhi ya
sehemu ya miili yao nje. Siyo sawa. Mwanamke staha. Anapaswa kujiheshimu
na kujihifadhi.
Kujianika na kujiacha wazi, kutakufanya uonekane mhuni, usiye na maana na hivyo hata kama ukifanikiwa kumnasa, fahamu kuwa mwisho wenu utaishia kwenye mapenzi tu na siyo ndoa.
Kujianika na kujiacha wazi, kutakufanya uonekane mhuni, usiye na maana na hivyo hata kama ukifanikiwa kumnasa, fahamu kuwa mwisho wenu utaishia kwenye mapenzi tu na siyo ndoa.
Ni vyema pia ukazingatia kuhusu mtindo wa nywele na vipodozi
kulingana na mahali ulipo.
Asante somo zuri sana.
JibuFuta