Mtandao wa Facebook umelaumiwa kwa kuwafanyia wateja wake utafiti wa kisaikolojia bila ya kuwajulisha.
Nia ya utafiti huo ilikuwa kujua kama wateja
wake wamebadili tabia ya kuweka picha na mawazo yao katika mtandao huo
kutokana na kukasirishwa na tabia za baadhi ya watumiaji wenzao.
Utafiti huo uliohusisha takribani
watumiaji 700,000 unaonyesha kuwa Facebook inacheza na taarifa za
watumiaji wake ili kupata hisia zao katika kile wanachokiweka kwenye
mtandao huo.
Hata hivyo mtandao wa Facebook umekanusha madai
hayo na kwamba hakuna mtumiaji binafsi aliyelengwa na utafiti huo
uliofanywa na mtandao huo kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Cornell na
California.
Ngoja tuuite utafiti kama Facebook wenyewe wanavyouita, lakini ni dalili za wazi za kushindwa kuzingatia maadili na nguvu ya kulinda haki za watumiaji wake
amesema Kate Crawford katika
ukurasa wake wa Twitter.
Waziri wa kazi Jim Sheridan mjumbe wa bodi ya
mawasiliano ameagiza uchunguzi kufanyikadhidi ya mtandao huo wa Facebook
katika tuhuma hizi.
Hata hivyo Katherine Sledge Moore, Profesa wa
Saikolojia katika chuo cha Elmhurst , Illinois amesema kwa jinsi ambavyo
Facebook wamekuwa wakishughulika na taarifa za wateja wake makubaliano
yaliyopo katika utafiti huo hadhani kama yapo nje ya hali ya kawaida.
Adam Kramer kutoka Facebook mmoja kati ya
walioandaa taarifa ya utafiti huo anasema wanadhani kuwa ilikuwa mhimu
kwao kutafiti mashaka yanayowakumba watumiaji hasa katika mawazo
yanayowekwa na marafiki zao na jinsi yanavyowafanya wafikirie tofauti .
0 comments:
Chapisha Maoni