Mwanamke aliyekuwa kinara wa mtandao uliokuwa
unawaingiza watoto wadogo katika biashara ya ngono amehukumiwa kifungo
cha miaka 12 jela nchini Uingereza.
Inaarifiwa Amanda Spencer, alifanya urafiki na
wasichana hao wadogo wengine wakiwa na umri wa miaka 13 kabla ya
kuwalazimisha kufanya ngono na wanaume na kisha kuwalipa.
Mahakama ya Shefield iliambiwa kuwa Amanda alitumia pesa zake kwa madawa ya kulevya na pombe.
Spenser mwenye umri wa miaka 23, alipatikana na
hatia wiki jana kwa makosa 16 yote yakihusishwa na biashara ya ngono kwa
watoto wadogo.
Hata hivyo mahakama ilifutilia mbali makosa
mengine 7 dhidi yake ikiwemo, kupanga na kufanikisha biashara ya ngono
miongoni mwa watoto, kuwalazimisha watoto kuwa makahaba na kuwatumia
vibaya watoto.
Wakati wa kesi hiyo, mahakama iliarifiwa kuwa Spencer aliwalenga watoto ambao walikuwa hawana uwezo.
Lakini Spencer alikana mashitaka yote dhidi yake
akisema kuwa waathiriwa walisema uongo na kwamba hajawahi kukutana nao
wala hawafahamu.
0 comments:
Chapisha Maoni