Msanii wa filamu za Kibongo, Meya Shaban ‘Aki wa Bongo Muvi’ ameachana
na ukapera baada ya kufunga ndoa na msanii mwenzake, Amina Shaban,
Ijumaa Wikienda lilikuwepo ndani ya nyumba.
Staa huyo wa Sinema ya Devil Kingdom ya mwigizaji Emmanuel Myamba
‘Pastor Myamba’ alifunga ndoa hiyo Ijumaa iliyopita kwenye Msikiti wa
Mbezi, Tanki-Bovu, Dar na kufuatiwa na bonge la sherehe katika Ukumbi wa
Mbezi Beach Park.
Katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na wanahabari wetu, ilipambwa na watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa filamu za Kibongo.
Shughuli hiyo ya kukata na shoka iliwashangaza watu kutokana na
maharusi hao majina ya baba zao kufanana huku wageni waalikwa wakisema
kwamba ikitokea hivyo ndoa huwa inadumu kwa muda mrefu.
Akizungumza mbele ya wageni waalikwa, Aki wa Bongo Muvi alisema kuwa
anamshukuru Mungu kwa kuwa ametimiza ahadi ya ndoa kwani mara ya kwanza
walikutana na mkewe kwenye Chuo cha TFTC cha Pastor Muyamba na kuanzisha
urafiki hadi wakafikia hatua hiyo ya ndoa.
Namshukuru sana Pastor Muyamba kwani ndiye mwalimu wangu wa sanaa na kama siyo sanaa, nisingempata mwanamke kama huyu, yaani siku ya leo nina furaha sana
alisema Aki wa Bongo Muvi ambaye ameandika historia kwa
tukio hilo.
Baadhi ya wasanii waliohudhuria kwenye sherehe hiyo ni Pastor
Muyamba, Zawadi, Nova ambaye alikuwa mshehereshaji na Rais wa Shirikisho
la Filamu la Tanzani (TAFF), Saimon Mwakifwamba ambaye aliwapongeza kwa
hatua hiyo ya kuingia kwenye ndoa huku akiwataka wasanii wengine kuiga
mfano wao.
Baadhi ya sinema alizoigiza Aki wa Bongo Muvi aliyezidiwa urefu
kiaina na mkewe ni pamoja na The Lost Sons, Sometime Yes, Sometime No,
Yes Madam, Devil Kingdom, Pastor Muyamba Temptation, Uncle Mpozemenye na
nyingine.
0 comments:
Chapisha Maoni