Maumivu ya tumbo wakati wa miezi mitatu ya kwanza ya mimba ni mojawapo
ya matatizo yanayolalamikiwa na kina mama wengi.Kuna matatizo mengi
ambayo yanahusiana tu na mimba, hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kwamba
hali yoyote ambayo husababisha maumivu katika mgonjwa asiyekuwa na
ujauzito inaweza pia kutokea kwa mama mjamzito, ingawaje historia na
uchunguzi vinaweza kuwa tofauti.
Kwa asili kutathmini maumivu ya tumbo kwa mama mjamzito ina
changamoto kwa sababu kichefuchefu, kutapika, na maumivu ya tumbo
hujitokeza mara nyingi kwa wajawazito wengi . Mfuko wa uzazi unapotanuka
unaweza kusukuma viungo vingine kando ndani ya tumbo, upungufu wa damu
na leukocytosis ni kawaida katika mimba ya kawaida na si viashiriwa
vya upungufu wa damu au maradhi. Mgonjwa ambaye mimba imetunga nje ya
mfuko kipimo cha ultrasound kinaonyesha majimaji na uchafu ndani ya
mfuko wa uzazi bila ushahidi wa mimba.
Kiinitete kinapojipandikiza katika kuta za ndani za mfuko wa uzazi
inaweza kusababisha maumivu ya tumbo , ambayo huchukua muda wa siku 1- 2
na kiasi kidogo cha damu ukeni. Mara nyingi kiasi hiki ni kidogo na
hutokea kati ya siku 6 -12 baada ya tarehe inayohisiwa mimba kutungwa ,
mara nyingi kipindi hiki hukaribiana na siku ambayo mwanamke alikuwa
anatarajiwa kuingia hedhi. Hivyo, wagonjwa mara nyingi hufanya makosa
kwa kufikiri kuwa wameingia katika siku zao kama kawaida.
Mimba
iliyotunga nje ya mfuko ni tatizo linaloongoza kusababisha maumivu kwa
kina mama wengi sehemu mbalimbali duniani. Tatizo hili linaweza
kubainika kwa kutumia Ultrasounda na kipimo cha homoni HCG. Hata hivyo
tatizo hili linatibiwa kama dharura kwa mama kufanyiwa upasuaji.
Sababu nyingine ni kutoka kwa mimba. Mimba inaweza kutoka yenyewe au
kutolewa kwa makusudi. Tatizo hili huambatana na maumivu pamoja na
kuvuja damu. Utoaji wa mimba usiokuwa salama unaongoza kusababisha vifo
vya kina mama katika nchi zinazoendelea.
Uvimbe
kwenye mirija ya mayai(Ovarian cyst). Wakati mwingine uvimbe huu
hupasuka au kujizungusha. Hata hivyo unaweza kupungua na usipopungua
unaweza kuondolewa kwa njia ya upasuaji hasa wakati wa muhula wa pili wa
ujauzito.
Sababu nyingine ni kujizungusha kwa mirija ya mayai(Ovarian torsion). Hii hujitokeza mara chache.
Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi pia husababisha maumivu hasa unapokuwa
mkubwa. Tatizo hili linaweza kusababisha ujauzito kutoka hasa katika
miezi ya awali.
Kidole tumbo(appendicitis) hujitokeza kwa uwiano sawa kama wanawake
ambao hawana ujauzito. Matibabu ya ugonjwa huu ni upasauji. Mara nyingi
wanawake wengi hupata uchungu baada ya upasuaji.
Kutokana na mabadiliko ya homoni wanawake wengi hupata tatizo la mawe
kwenye mfuko wa nyongo. Tatizo hii huweza kugunduliwa kwa njia ya
ultrasound.Matibabu hutegemea na dalili.
Uvimbe(inflammation) kwenye mfuko wa nyongo ni tatizo la ghafla
linalosababisha maumivu makali ambalo pia hujitokeza wakati wa mimba.
Tatizo hili mara nyingi husababishwa na mawe kweny mfuko wa nyongo.
Antibiotics hutumika katika matibabau ya uchongo huu.
Wanawake wengi wakati wa hujauzito hupata maambukizi kwenye njia ya
mkonjo mara kwa mara. Hii ni kutokana na mabadiliko yanayojitokeza
wakati huu wa mimba.
Sababu nyingine ya maumivu husababishwa na ROUND LIGAMENT. Ligament hii
ndio inayoshikilia mfuko wa uzazi tumbo. Mfuko wa uzazi unavyozidi
kukua, ligament hii huvutika na kusababaisha maumivu.
Dawa za maumivu husaidia kwa tatizo hili.
Ultrasound hutumika katika uchunguzi wa maumivu ya tumbo wakati wa
ujauzito. Kongosho, mfuko wa nyongo na kidole tumbo vyote huonekana kwa
mama mjamzito. Vipimo vinavyotumia mionzi viyumike tu pale
inapohitajika kwa mama mjamzito.
0 comments:
Chapisha Maoni