Ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za binadamu nchini Tanzania imesema watoto wapatao 800 walilawitiwa nchini humu mwaka 2013.
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika hilo kumekuwa na
ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto nchini
Tanzania ambapo kumi kati yao wakiwa wamefanyiwa ukatili huo na wazazi
wao wenyewe.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza
anasema ripoti hiyo ya haki za binadamu kwa mwaka 2013 iliyotolewa mjini
Dar es Salaam, imebainisha hayo kutokana na utafiti uliofanywa na Kituo
hicho cha sheria na Haki za binadamu -LHRC kwa pamoja na kituo cha
huduma za sheria Zanzibar.
Akiongea na BBC Mkurugenzi mtendaji wa taasisi
hiyo Dr Helen Kijo-Bisimba, amesema watoto wamekuwa katika maisha ya
hatari Zaidi nchini humo kutokana na watu wa karibu wakiwemo wazazi wa
kiume na hata kaka na wajomba zao kubainika wanawafanyia vitendo vya
ubakaji.
Ripoti hiyo ambayo ni ya 11 kutolewa na taasisi
hiyo imebainisha kuwepo kwa matukio ya raia kuwaua raia wenzao ambayo
yameongeza kasi za ukiukwaji wa haki za kuishi nchini humo.
Aidha utafiti huo umeonyesha kuwa watu zaidi ya
1600 wakiwemo askari polisi wanane, waliuawa na wananchi wenye hasira
kali katika matukio tofauti, huku askari polisi nao waliwaua raia 28
katika kipindi cha mwaka 2013.
0 comments:
Chapisha Maoni