LICHA ya hivi karibuni gazeti dada la hili, Risasi
kumnukuu mcheza filamu mahiri Vincent Kigosi ‘Ray’ akikana kuwepo kwa
mpango wa kumuoa mpenzi wake Chuchu Hans, dada huyo ambaye pia ni msanii
wa fani hiyo, ameibuka na kusema piga ua lazima wataoana.
Akizungumza na mtandao huu juzikati, Chuchu alisema hana uhakika kama
mpenzi wake huyo alimaanisha kile kilichoandikwa gazetini kwa vile ana
mapenzi ya dhati kwake.
“Kiukweli mimi moyo wangu unakataa kama alisema maneno hayo kwa vile ni mtu ambaye namjua ana mapenzi ya dhati kwangu,”
alisema.
Mwanadada huyo aliongeza kuwa, anahisi kuna kidudu mtu mwenye nia ya
kuleta mtafaruku ndani ya uhusiano wao kwa kuchochea fitina ili mapenzi
yao yavurugike.
“Unajua kuwa kuna uwezekano kabisa kuna kidudu mtu ambaye anataka kuleta mtafaruku ili tugombane bila sababu na hilo mimi sikubaliani nalo,”
alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni