Mtanzania aliyejulikana kwa jina la Sabrina au Habiba
kwamba, aliondoka Bongo kwenda Guangzhou, China akidanganywa na mwanamke
mmoja kwamba anakwenda kufanya kazi kwenye saluni ya kike.
Habari zilisema baada ya kufika China, mwanamke huyo alimnyang’anya
Habiba hati ya kusafiria na kumwingiza kwenye biashara ya ukahaba kwa
kumuuza kwa wanaume huku ujira akiuchukua yeye.
Ilidaiwa kuwa, tabia hiyo ndiyo iliyopo kwa sasa kwamba, kuna wasichana wanachukuliwa kupelekwa nchini humo kwa kudanganywa kufanya kazi saluni matokeo yake huishia kwenye ukahaba.
Ilidaiwa kuwa, tabia hiyo ndiyo iliyopo kwa sasa kwamba, kuna wasichana wanachukuliwa kupelekwa nchini humo kwa kudanganywa kufanya kazi saluni matokeo yake huishia kwenye ukahaba.
Ndugu
mmoja aliyejitambulisha kuwa ni kaka wa marehemu na kusema kuwa wamesoma habari za kifo cha Habiba kwenye Gazeti la
Ijumaa Wikienda.
Akizungumza kwa sauti iliyojaa simanzi, ndugu huyo alisema nyumbani kwao ni Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza msibani, baba mzazi wa marehemu, mzee Yusuf Ally alisema Habiba aliondoka nchini kwa kutoroka kwenye Sikukuu ya Idd El Haj mwaka 2012.
Akizungumza msibani, baba mzazi wa marehemu, mzee Yusuf Ally alisema Habiba aliondoka nchini kwa kutoroka kwenye Sikukuu ya Idd El Haj mwaka 2012.
Alisema hakuwa na mawasiliano mazuri na bintiye huyo si kwa sababu ya
kutoroka tu bali kwa vitendo alivyokuwa akivifanya na kila alipomuonya
binti huyo hakusikia, mwishowe akaamua kukata mawasiliano naye.
“Sikuwa na mawasiliano na Habiba tangu Machi 2010 kwani aliniudhi
sana,” alisema mzee huyo licha ya kwamba alikuwa akiporomosha machozi
kufuatia taarifa za kifo cha binti yake.
Akiendelea kusimulia maisha aliyokuwa akiishi na mwanaye huyo, mzee Yusuf alisema:
“Habiba alibadilika tabia akawa hataki kusoma. Mbaya zaidi kilichonikera ni pale alipokataa kwenda kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2010. Kiukweli iliniuma sana.
“Habiba alibadilika tabia akawa hataki kusoma. Mbaya zaidi kilichonikera ni pale alipokataa kwenda kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2010. Kiukweli iliniuma sana.
“Nilimsomesha kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, nilikuwa
najinyima kula kwa ajili yake, siku ya mtihani akakataa kwenda shule,
niliumia sana hasa nikikumbuka fedha zangu nilizotupa kwa ajili yake,”
alisema.
Naye dada wa Habiba,
Aziza Said ambaye alikuwa akiishi na marehemu alisema kwamba ilikuwa
siku ya Idd El Haj mwaka 2012 ndiyo siku ambayo mdogo wake huyo
alitoroka nyumbani na kwenda kujificha kusikojulikana.
“Siku hiyo nilimwachia fedha ili aende saluni akamsuke mtoto, mi
nikaenda Kariakoo. Niliporudi nikakuta fedha za kusukia ziko mezani na
mtoto anacheza nje.
“Nilimuuliza mwanangu mama mdogo yuko wapi? Akanijibu hajui. Sikuwa
na wasiwasi kwani nilijua alikwenda kwa mashoga zake kula sikukuu,
kwangu alihisi ningembana. Kumbe mwenzangu yuko katika mipango ya
kutoroshwa nchini,” alisema dada huyo na kuangua kilio.
Familia hiyo
ilisema mwanamke aliyemtorosha Habiba kutoka Bongo kwenda China wanamjua
(jina tunalo) kwani waliwahi kuishi naye nyumba moja, Manzese jijini
Dar lakini wakawa hawaongei naye kwa sababu ya tabia zake mbaya.
Walisema mwanamke huyo alianza kumbadili tabia Habiba miezi michache
kabla ya safari ya China, hasa kwa mavazi ya ajabu na tabia ya kutotulia
nyumbani.
Waliendelea kusema kuwa, ilifika mahali kutokana na tabia yake mpya
isiyo na maadili, waliamini binti huyo ametumbukia kwenye mambo ya
kigodoro (ngoma za uswahilini).
Kaka wa
marehemu Mohammed Yusuf Ally alipoongea na Fichuo Tz hili msibani hapo
alisema kuwa mara ya mwisho kufanya mawasiliano na marehemu ilikuwa
Valentine’s Day (Sikukuu ya Wapendanao) – Februari 14, mwaka huu,
ambapo alimtumia ujumbe mfupi wa maneno katika Mtandao wa Kijamii wa
WhatsApp lakini meseji hiyo haikujibiwa.
“Nimeshtuka sana leo kupata taarifa kwamba mdogo wangu amefariki
dunia tena baada ya kusoma gazeti (Ijumaa Wikienda) huku kifo chake
kikiwa cha kikatili kiasi hicho,” alisema akilia kaka huyo.
Kwa mujibu wa
ndugu, mbali na miongoni mwao kulisoma Gazeti la Ijumaa Wikienda na
kupata taarifa, lakini kwa mzee Yusuf habari zilimfikia baada ya jirani
kununua gazeti hilo na kumpelekea nyumbani hapo.
“Nalishukuru hili gazeti
(Wikienda) kwani bila ya wao kuandika tusingejua nini kinaendelea huko
China,” alisema kaka wa marehemu huku akiwa ameshika gazeti hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni