Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Thadeus Ruwa’ichi
amewaonya wasanii kuwa maigizo yao yasilenge kuchafua umma ama kikundi
chochote kwani wanaweza kuleta mgawanyiko katika taifa.Akizungumzia
msimamo wa kanisa kuhusiana na filamu ya Sister Maria ya mwigizaji
Vincent Kigosi ‘Ray’ ambayo kanisa hilo liliipinga kutokana na madai ya
kukiuka maadili, Askofu Ruwa’ichi alisema hawakubalini nayo kwani mavazi
ya masista yaliyotumiwa na wasanii hao, yalitumika vibaya hivyo
hawakubaliani nayo.
Akifafanua zaidi kuhusiana na filamu hiyo,
kiongozi huyo wa kiroho alisema alisononeshwa na kazi hiyo ambayo
ilikuwa na dosari za kuingilia imani ya kikatoliki kwani mavazi ya
kanisa yalitumika kuvaliwa bila staha.
“Ile filamu ilikuwa na lengo la kuhatarisha jamii, kamwe isiendelee
kwani ni hatari kwa watu ama mtu binafsi anayechukizwa na tatizo hilo,
“Maigizo yanayofanywa yanaweza kuwa na lengo la kutumbuiza, lakini
kutumbuiza kokote kule, hakupaswi kuhatarisha lengo la kulea ama
kuvuruga mambo ya watu fulani, kulinda heshima ya watu binafsi ama
taasisi, nidhamu inahitajika kwa kila jambo wanalolifanya,” alisema.
Askofu
huyo alisema taifa lina mambo mengi na linajivunia kwa amani ya muda
mrefu, hivyo waigizaji hao wanapoigiza maigizo ambayo yanagusa imani au
jamii ya watu wengine linaweza kuwa tatizo kubwa huko mbele.
“Hakuna haja ya maigizo kuchafua watu wengine, heshima kwa wote ni
jambo jema ambalo linaweza kuongeza upendo kwa kila jambo ufanyalo kwa
jamii nyingine.
“Wakifanya kazi zao kwa ufasaha bado taifa litawaheshimu, hakuna mtu ama kundi ambao wangependelea kutokee vurugu eti kwa sababu ya maigizo ya mtu fulani, haiwezi kuungwa mkono,” alisema askofu huyo.
“Wakifanya kazi zao kwa ufasaha bado taifa litawaheshimu, hakuna mtu ama kundi ambao wangependelea kutokee vurugu eti kwa sababu ya maigizo ya mtu fulani, haiwezi kuungwa mkono,” alisema askofu huyo.
0 comments:
Chapisha Maoni