SAKATA la kujinyonga kwa msanii wa filamu Bongo, Victor Peter
limegubikwa na matukio tofauti ya kustaajabisha ambayo marehemu
aliyafanya siku kadhaa kabla hajapatwa na umauti, Ijumaa limefukunyua
kila kitu.
Kwa mujibu wa rafiki wa marehemu, Hamisi Koba, msanii huyo
alijinyonga usiku wa Februari 27, mwaka huu mkoani Tanga ambapo marehemu
alifika jijini humo kuigiza filamu yake iitwayo Our Family.
Hamisi alisema Victor aliwasili jijini humo akiwa na timu ya wasanii
sita na kufikia kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Safari Junior
iliyopo maeneo ya Kisosora ambapo punde walianza kushuti filamu hiyo
ambayo yeye na Mzee Jengua ndiyo walikuwa wahusika wakuu.
“Mimi ndiye nilikuwa kama mwenyeji wake mkubwa hapa Tanga, alikuwa ni
mpole na siku zote tulipokuwa kazini kwa ajili ya kushuti filamu hiyo
aliniambia mambo mengi kuonesha amejipanga kuhakikisha anaifikisha
mbali.
“Victor alitokea Mwanza, akaenda Dar ambapo alifika na kuandaa filamu
yake ya kwanza aliyoiita Chozi ambayo tayari ilikuwa imekamilika na
kuiuza kwenye Kampuni ya Kapiko ya jijini humo,” alisema Koba na
kuongeza:
“Filamu hiyo ilikuwa bado haijatoka, akaamua kuja Tanga kuandaa
filamu hiyo ya pili ambayo nayo ilikamilika juzi. Naumia sana
ninapokumbuka mipango yake maana alikuwa ana ndoto za kufanya makubwa.
“Siku ya Januari 27 tulipokuwa tunakamilisha filamu, kuna muda
alikuwa anaonekana kama ana wenge hivi... alipomaliza kushuti sehemu
yake tulienda benki, akachukua fedha na kuwalipa wasanii wote.”
Akiendelea kutiririka juu ya tukio hilo, Koba alisema marehemu
alionesha kama alikiona kifo chake kabla kwani aliuliza mara mbilimbili
kama kuna mtu anamdai ili amlipe.
“Wakati anatupatia fedha kila mara alikuwa anauliza kama kuna mtu
anamdai hadi tuliingiwa wasiwasi na ingawa wengine walisema atakuwa
amefurahia labda kumaliza muvi yake,” alisema.
Koba alizidi kueleza kuwa, marehemu akiwa na furaha ya kumaliza muvi
hiyo, alikwenda chumbani kwake na kujifungia lakini alfajiri (Januari
28) walipomgongea mlango waligundua amejinyonga.
“Tulichungulia kupitia tundu la funguo tukaona kama ananing’inia
ndipo tukaenda kwenye kituo cha Polisi cha Chumbageni na kuchukua askari
ambao walishirikiana na mwenye gesti hiyo kuvunja
mlango na kumkuta kajinyonga, tukachukua mwili na kuupeleka kwenye Hospitali ya Bombo, mipango ya kuusafi risha mwili kwenda Kahama nyumbani kwao imeanza,” alisema Koba na kuongeza:
mlango na kumkuta kajinyonga, tukachukua mwili na kuupeleka kwenye Hospitali ya Bombo, mipango ya kuusafi risha mwili kwenda Kahama nyumbani kwao imeanza,” alisema Koba na kuongeza:
“Kwenye hiyo filamu yake, stori ilikuwa mzee Jengua kama baba wa
Victor ambapo Mzee Jengua alikufa na baadaye Victor anakufa kiajabu,
kifo kimempata kweli.”
Kuhusiana na kifo hicho, Koba alisema kilimuuma kwani alikilinganisha
na kile kilichomtokea marehemu Steven Kanumba ambaye pia aliigiza
filamu ya Power of Love ikionesha anakufa, akafa kikwelikweli.
Mwili wa marehemu uliokuwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Bombo
ulitarajiwa kusafi rishwa juzi kwenda nyumbani kwao Kahama kuzikwa.
0 comments:
Chapisha Maoni