Jumatatu, Februari 01, 2016

RASMI! DAR ES SALAAM INA WILAYA TANO SASA

RAIS Dk. John Magufuli ameidhinisha kuwepo kwa wilaya tano katika jiji la Dar es Salaam, badala ya tatu zilizokuwepo awali, ili kuleta maendeleo ya haraka hususan katika elimu. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, alisema jana kuwa, waliwasilisha ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke kwa rais, ambapo ameshaliidhinisha.
“Hatua hii ya kuwepo kwa wilaya tano italiwezesha jiji la Dar es Salaam, kupata maendeleo ya haraka kwa kugawanywa kwa wilaya hizo, ambapo kutakuwa na usimamizi thabiti na hakutakuwa na kisingizio cha kuelemewa kwa majukumu kwa watendaji,”alisema.
Aliomba katika ugawaji wa wilaya hizo, rasilimali zilizopo na mipaka igawanywe kwa manufaa ya wananchi wa wilaya hizo. Aidha, alisema kinachosubiriwa ni ugawaji wa mipaka na kutangazwa rasmi kuongezeka wilaya mbili ya Kigamboni na Ubungo na kufi kisha idadi ya wilaya tano katika jiji la Dar es Salaam.
Kutokana na kuongezeka kwa wilaya, Sadiki aliwataka watendaji wake kuwa waadilifu katika ugawaji wa mipaka na rasilimali zilizopo ili kuleta maendeleo yaliyokusudiwa.
Akizungumzia ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke, Sadiki alisema hadi kufi kia jana, ombi hilo lilishaidhinishwa na rais, hivyo Kinondoni itakuwa na wilaya mbili za Kinondoni na Ubungo huku wilaya ya Temeke ikiwa na wilaya za Temeke na Kigamboni.

0 comments:

Chapisha Maoni