Jumatano, Januari 06, 2016

UMEWAHI KUMSIKIA 'MR. PLASTIC FANTASTIC'? YUPO PIA KATIKA KITABU CHA THE GUINNESS

Huku akiwa amekusanya kadi za mkopo 1,497 au "credit cards" na kuhitimu mkopo wa hadi dola milioni moja nukta saba (dola milioni 1.7),Walter Cavanagh, ambaye amekuwa katika kitabu cha "Guinness Book" tangu mwaka wa 1971 sasa anashikilia rekodi kwa kuwa na kadi nyingi na kibeti ndefu zaidi kote duniani.
Sifa hiyo imepelekea Cavanagh kupewa jina la utani la "Mr. Plastic Fantastic" kwa kukusanya kadi hizo, ambazo huwa zimetengezwa na plastiki. "Mr. Plastic Fantastic" alianza kukusanya kadi hizo mwaka wa 1960 waliposhindana na mfamasia mwenzake kukusanya kadi hizo.

0 comments:

Chapisha Maoni