Ijumaa, Januari 29, 2016

UHOLANZI YAONGEZA NGUVU KUWAPIGA ISIS

Nchi ya Uholanzi siku ya Ijumaa (Jana) iliamua kujiunga na mashambulizi yanayoongozwa na nchi ya Marekani dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State (ISIS) nchini Iraq na Syria.
"Tukiweza kuyamaliza maficho ya kikundi hiki yaliyoko Iraq na Syria pia tutaweza kuzuia mashambulizi," Waziri Mkuu Mark Rutte kutoka Uholanzi alisema katika mkutano wa waandishi wa habari.
Baraza la mawaziri wa Uholanzi pia wamekubali hatua ambazo zitatumiwa kutatua migogoro huko Iraq na Syria kwa njia ya kisiasa na kibinadamu.

0 comments:

Chapisha Maoni