Ijumaa, Januari 15, 2016

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 15.01.2015

Baada ya kupewa adhabu na Fifa - Real Madrid wanapanga kutumia pauni milioni 250 katika dirisha la usajili la Januari,-- milioni 80 zikiwa za kumsajili Eden Hazard wa Chelsea, wanawataka pia kipa wa Manchester United David de Gea, Paul Pogba wa Juventus, Robert Lewandowski wa Bayern Munich na mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero (Sun) mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane na beki John Stones wa Everton pia wanasakwa na Real Madrid (Daily Star),hata hivyo adhabu waliyopewa Real, hawataweza kuwachukua David de Gea na Eden Hazard (Independent), meneja wa Leicester, Claudio Ranieri anataka kumsajili mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino (Daily Mirror), hata hivyo West Brom wamesema Berahino hauzwi na wamewaonya Tottenham na Newcastle kutopanda dau (Telegraph), Chelsea wanakaribia kumsajili Alexandre Pato kutoka Corinthians (ESPN Brazil), Chelsea watalazimika kutoa pauni milioni 10 kumpata mshambuliaji huyo (Telegraph), meneja wa Chelsea Guus Hiddink ameambiwa amuuze kwanza Lioc Remy kabla ya kumnunua Pato (Daily Star), Chelsea wanaamini matumaini yao ya kumpata Diego Simione yameongezeka baada ya Atletico Madrid kupewa adhabu ya kutosajili (Daily Mirror), West Ham wana matumaini ya kuwazidi kete Everton katika kumsajili beki wa kulia wa Leeds United Sam Byram (Daily Express), Leicester City wanakaribia kumsajili beki kutoka Ghana Daniel Amartey kutoka FC Copenhagen (Sun), Newcastle wako tayari kutoa pauni milioni 12 kumsajili Andros Townsend kutoka Tottenham (Sun), Marseille wanakaribia kumsajili kwa mkopo hadi mwisho wa msimu, winga wa Newcastle Florian Thauvin (Times), Liverpool na Tottenham wanamfuatilia winga Yasin ben el-Mhanni (Daily Mail), Manchester United wanakaribia kufanya usajili wa kwanza kwa kumchukua beki wa kati kutoka Italia, Luca Ercolani, 16, kutoka klabu ya Forli (Daily Express), kiungo wa Tottenham Delle Alli huenda akasaini mkataba mwingine mpya mwisho wa msimu, klabu hiyo ikitekeleza sera zake za kuwazawadia wachezaji wao bora (Times)

NA Salim Kikeke

0 comments:

Chapisha Maoni