Jumanne, Januari 19, 2016

STAMIGOLD BIHAMURO NDIO MGODI PEKEE UNAOSIMAMIWA NA WATAALAM WAZAWA

Mgodi wa Stamigold Biharamulo ni mgodi pekee hapa nchini unaozalisha dhahabu kwa kusimamiwa na kuendeshwa na Wataalam wa Kitanzania pekee. Mgodi wa Biharamulo chini ya Meneja wake Mkuu Mhandisi Dennis Sebugwao, umeweza kuisaidia serikali kupunguza tatizo la ajira wakati huo huo kuiongezea serikali mapato kutokana na kodi mbalimbali zinazolipwa na Wafanyakazi walioajiriwa (PAYE)
Mbali na kuajiri Wataalam wa fani mbalimbali mgodi pia unatumia Wakandarasi wa Kitanzania pamoja na kutoa ajira za muda mfupi kwa wakazi wa vijiji vilivyo jirani na mgodi. (Mavota & Mkunkwa)
Wengi wa Watanzania wana ile dhana ya kuwa Watanzania hatuna uwezo wa kusimamia na kuendesha migodi bila kuajiri wataalamu kutoka nje ya nchi. Mgodi wa Stamigold Biharamulo umedhamiria kuendelea kudhihirishia Watanzania wenzetu na dunia nzima kwa ujumla kuwa kupitia wataalamu tulionao nchini kwetu tunao uwezo wa kuzalisha dhahabu bila kutegemea wataalamu kutoka nje ya nchi.
“Tutaendelea kufanya kazi kwa uadilifu, weledi, ushirikiano, bila kukata tamaa na bila kushindwa. Daima tutasonga mbele kurudi nyuma ni mwiko.”

0 comments:

Chapisha Maoni