Jumapili, Januari 17, 2016

NETANYAHU ALAANIWA KWA KUTAKA KUPIGA MARUFUKU ADHANA


Wanaharakati wa kisiasa Palestina wamekosoa vikali matamshi yaliyojaa ubaguzi ya Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel ambaye ametaka kupigwa marufuku kusomwa adhana kwa vipaza sauti katika misikiti huko Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel katika mkutano na chama cha Kizayuni cha Likud amedai eti kuwa adhana inawakera wengine.
Netanhayu anataka kupitishwa sheria za kibaguzi ili kuzuia kusomwa adhana kwa vipaza sauti katika ardhi za Palestina zilizokaliwa kwa mabavu na Israel mwaka 1948.
Kufuatia matamshi hayo, Ibrahim Abu Jaber, mwanaharakati wa kisiasa Palestina amesema si mara ya kwanza kwa utawala wa Kizayuni kujaribu kuweka vizingiti katika kusomwa adhana kwa vipaza sauti. Amesema miaka kadhaa iliyopita utawala wa Kizayuni ulitaka kupunguzwa sauti ya adhana misikitini.
Ameongeza kuwa kuweka vizingiti vya kidini katika ardhi za Palestina zilizokaliwa kwa mabavu mwaka 1948 ni katika sera za kufurutu ada za Israel. Amesema Wazayuni wanaitazama misikiti kama vituo vya uchochezi dhidi ya utawala huo ghasibu. Abu Jabir amesema matamshi hayo ya Netanyahu ni katika fremu ya kuondoa utambulisho wa Kiarabu na Kiislamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ili kuasisi dola la Kiyahudi.

0 comments:

Chapisha Maoni