Alhamisi, Januari 21, 2016

MCHUNGAJI AMCHOMA MOTO MUUMINI AKIAMINI HAUTOMUUNGUZA

Jumapili iliyopita ndani ya kanisa moja lililopo mtaa wa Unity wilayani Abule nchini Nigeria, baada ya mchungaji ‘kumchoma’ moto muumini mmoja wa kanisa lake akidai ni maono aliyooteshwa na Mungu.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, mchungaji huyo alianza kwa kuwaambia waumini kuwa ameoteshwa kuwepo kwa nguvu kubwa ya Mungu mahali hapo, ambayo hata akiamua kumchoma muumini moto hawezi kuungua kwa kuwepo na nguvu kubwa iliyokuwepo.
Unaambiwa ndipo akajitokeza muumini mmoja wa kike aliyejulikana kama Madam Bosede, kwa nia ya kutaka ‘apigwe’ moto ili kuonesha mfano wa nguvu ya Mungu.
Baada ya kumwagia mafuta ya taa na kuanza kumchoma moto, ndipo mambo yalipogeuka baada ya Bosede kuanza kuungua vibaya na kuomba msaada.

0 comments:

Chapisha Maoni