Alhamisi, Januari 14, 2016

MAALIM SEIF WA CUF AMTUMIA BARUA PAPA FRANCIS KUNUSURU SIASA ZA ZANZIBAR

Aliyekuwa Mgombea Urais wa CUF, Maalim Seif amemwandikia barua kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis akimuomba kutumia ushawishi wake na Tanzania kumaliza mzozo wa kisiasa kisiwani humo kabla hali haijawa mbaya.
Amemweleza Papa Francis kuwa baadhi ya shughuli za kiuchumi zimesimama kutokana na wananchi wengi kuwa na hofu kuhusu mustakabali wa nchi yao.

Maalimu Seif sasa amwangukia Papa Benedict uchaguzi Z'bar.Na Waandishi wetu14th January 2016B-pepeChapaMakamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, amemwangukia Papa Benedict XVI kwa kumwandikia barua, akimuomba kutumia ushawishi wake na Tanzania kumaliza mzozo wa kisiasa kisiwani humo kabla hali haijawa mbaya.Kwa mujibu wa barua yake ya Novemba 25, mwaka jana ambayo gazeti hili imefanikiwa kuona nakala yake, Maalim Seif alimwomba Papa kutumia ushawishi alionao kwa serikali ya Tanzania ili kuhakikisha haki inatendeka na kuepusha vurugu zinazoweza kutokea.
ilisema barua hiyo.
Barua hiyo ya Maalim Seif ilisema, Zanzibar ina mchanganyiko wa Waislamu na Wakristo, hivyo hakuna mgawanyiko kwa misingi ya udini lakini hatua ya wananchi kukosa haki yao ya kidemokrasia kupitia sanduku la kura baada ya miaka 20 ya chaguzi visiwani humo kunaweza kusababisha vijana ambao hawafurahishwi na mwenendo huo kutumia njia mbaya kutafuta haki yao.
ilisema.
ilisema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Papa.
Iliongeza kuwa, Zanzibar ilipopata Uhuru wake mwaka 1963, kwa kiwango kikubwa watu wake waliishi kwa amani na ushirikiano baina ya watu wa madhehebu yote ya Katoliki, Anglikana, Sunni, Shia na Hindu na hakukuwahi kuwa na mgogoro wala hofu ya watu hao kuhitilafiana kwa misingi ya tofauti ya dini.
Ilisema Chama cha Wananchi CUF

kimekuwa kikishinda chaguzi zote tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, lakini haijawahi kupewa ushindi wake hata muhula mmoja.
“Ni wiki tatu sasa tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu na hali hii imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli za kuichumi kutokana na wananchi wengi kuwa na hofu kuhusu mustakabali wa hali hii….watu wanashindwa kujua nini kitatokea maana wana hofu kwamba hali hii inaweza kuharibu umoja wa kitaifa kwa watu kuishi kwa upendo bila kujali dini wala kabila,” 
“Badala ya kuchukua hatua za pamoja kuzuia uovu huu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo chama chake kilishinda kwenye uchaguzi mkuu uliopita, imekuwa ikisaidia serikali ya Zanzibar kwa kutumia askari na majeshi yake kutishia watu wa upinzani,” 
“Wakati mmishenari wa kikristu alipomuomba Sultan wa Zanzibar mwaka 1840 kibali cha kujenga asasi ya kusaidia jamii kwenye eneo lake, Sultani yule ambaye alikuwa Muislamu alimtambua kama mtumishi wa Mungu aliyekuwa na lengo la kuendeleza neno la Mungu” 
NIPASHE

0 comments:

Chapisha Maoni