Uchumi wa Tanzania ulishuka kwa kiwango cha asilimia 6.8 mwezi wa Desemba mwaka uliopita kutoka asilimia 6.6 kama ilivyorekodiwa mwezi wa Novemba 2015.
Mfumuko huo ulisababishwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa katika kipindi cha mwaka uliokamilika Desemba 2015, tume inayosimamia takwimu nchini hapa (NBS) imesema.
Kulingana na mkurugenzi mkuu wa tume hiyo Ephraim Kwesigabo, bei ya mchele ilipanda kwa asilimia 4.7 katika kipindi hicho, huku bei ya mahindi ikipanda kwa asilimia 2.1 na bei ya unga kupanda na asilimia 2.1.Bidhaa zingine ambazo bei zao ziliongezeka ni pamoja na nyama kwa asilimia 2.6 na viazi kwa asilimia 3.9.




0 comments:
Chapisha Maoni