Mahakama Kuu kupitia Mheshimiwa Jaji Ignas Kitutsi asubuhi ya leo imetupilia mbali Maombi Madogo ya Kesi ya kuomba kupunguziwa gharama za dhamana ya kesi (security for cost) iliyofunguliwa dhidi ya mbunge wa Mikumi Mhe. Joseph Haule, maarufu kama Prof. Jay na mpinzani wake Jonas Nkya. Mahakama kuu imetupilia mbali kesi hiyo na kukubaliana na hoja za mapingamizi ya kisheria yaliyowekwa na jopo la Mawakili wa Joseph Haule, lililoongozwa na Tundu Lissu na John Mallya. Mahakama pia imemuamuru mlalamikaji alipe gharama zote za kesi na usumbufu.



0 comments:
Chapisha Maoni