Jumanne, Januari 19, 2016

KIASI CHA $ MIL. 693.1 NA EURO MIL. 369.6 ZA BANDIA ZILIZOKAMATWA KENYA

Raia wawili wa kigeni wamefikishwa mbele ya mahakama nchini Kenya kwa kushukiwa kuhusika na fedha bandia za kigeni.
Mkuu wa polisi nchini kenya ,Inspekta Jenerali , Joseph Boinnet alisema polisi walipata fedha bandia zenye thamani ya dola milioni 693.1 na Euro milioni 369.6 pamoja na mashine ya kuchapisha fedha kutoka washukiwa.
Boinnet, alisema Ousman Ibrahim Bako kutoka Cameroon na Mohammed Sani kwa jina ingine "Mustafa" kutoka Nigeria ni viongozi wakubwa watuhumiwa katika uchapishaji wa fedha bandia za kigeni.
Pesa zilizopatikana ni sawa na Shilingi 110 bilioni za Kenya ambazo ni sawa na Shilingi trilioni 2.3 za Tanzania.

0 comments:

Chapisha Maoni