Jumapili, Januari 10, 2016

FURAHI KIDOGO: HUU NI UJUMBE TOKA KWA MWANAUME KWENDA KWA 'FUTURE WIFE' AMBAYE HAJAMFAHAMU BADO

Kila siku kinatokea kipya duniani, hii ni kutoka hapa Tanzania, sijajua kama imechukuliwa mahala ikatafsiriwa, la-khasha ila nimeona nikushirikishe msomaji wangu juu ya ujumbe huu ufurahi na kuongeza oxygen kidogo kwenye ubongo wako, ni kutoka kwa mwanaume kwenda kwa 'future wife'.

Mke wangu mtarajiwa, najua uko sehemu salama na ukivuta muda na jamaa mwingine kabla hatujaoana. Lakini kabla sijakuweka ndani Ninayo machache ya kukueleza....1. My future wife, Jiandae kuwa mother material wala sio mom material.. usipaniki!!! .. ntakuelewesha nachomaanisha, Mke wangu mpendwa mmeo, ntakuwa father wala sio daddy kwa watoto wetu, usishangae nitawalea watoto wetu katika malezi ya tamaduni za kiafrika zaidi, hivyo kwa hilo ntakuwa conservative. Ningependa kukuonaukiwa mother wala sio mom ukawalea watoto kwa tamaduni za kigeni..2. My future wife, ntakuoa kutokana na uzuri wa asili uliojaaliwa na Mungu, hivyo bhas usitarajie kupata wasaa wa kujipachika kope na kucha za bandia wala mawigi (nywele za marehemu)..3. My future wife, huko uliko ni vyema ukaanza kujifunza kuendesha biashara na kusimamia, mmeo siamini katika kuajiriwa Bali kujiajiri..4. My future wife Siku tutakayokula kiapo kanisani, tutafanywa kuwa mwili mmoja, hivyo bhasi nisingependa tuje kutenganishwa na password kwenye simu zetu (no passwords)..5. My future wife, madhehebu yote hukiri kuwa MUNGU ni mmoja tu, hivyo bhasi nisingependa kukushuhudia ukihama madhehebu mbalimbali kutafuta ukombozi kwa MUNGU yuleyule..MY FUTURE WIFE, msalimie sana huyo mnayevuta nae muda kwa kwenda $amaki $amaki, Nyama Choma na Fiesta, mie ntakupeleka kanisani na kukuweka ndani.

0 comments:

Chapisha Maoni