Jumatatu, Januari 18, 2016

FUNDI SEREMALA ALIYEINGIZWA KATIKA KITABU CHA THE GUINNESS KWA KUWA NA VIDOLE 28

Raia wa Himatnaga, Gujarat nchini India, Devendra Suthar amebainika kuwa ndiye mtu aliye hai mwenye vidole vingi zaidi vya mikononi na miguuni. Devendra ambaye ni fundi seremala ana vidole 14 vya mikono na 14 vya miguuni hivyo jumla kuwa na vidole 28 hivyo kuweka rekodi katika Kitabu cha Kumbukumbu cha Dunia cha Guinness.
Ingawa katika shughuli zake za useremala vidole hivyo havimsumbui wala kumkwamisha katika ufanyaji wa kazi, lakini huwa makini sana katika shughuli za ukataji wa vitu mbalimbali.

0 comments:

Chapisha Maoni