Alhamisi, Januari 14, 2016

BAADA YA KUACHANA NA CHRIS BROWN, NINI KARRUECHE ANAKIFANYA NA CHRISTINA MILLAN? WAMENASWA!!

Mwigizaji na mwanamitindo wa nchini Marekani, Karrueche Tran jana jioni alinaswa akidendeka na mpenzi wake wa kike Christina Milian katika Klabu ya The Nice Guy iliyopo magharibi mwa Hollywood nchini Marekani.
Warembo hao waliweka wazi mahusiano yao mwaka jana baada ya Karrueche kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, mwanamuziki Chris Brown huku Christina akiwa tayari amembwaga mpenzi wake wa zamani mwanamuziki Lil Wayne.
Mbali na mahusiano hayo, lakini inaonyesha Karrueche mwenye umri wa miaka 27 bado anapambana na changamoto za maisha ya mapenzi ya jinsia moja kitendo kilichopelekea jana aandike katika ukurasa wake wa Twitter kuwa kwa sasa amefungua milango ya mahusiano mapya na kwamba yupo tayari kumpokea mpenzi baada ya kukaa mpweke kwa muda mrefu japo alidai itakuwa vigumu kumpata mpenzi wa kweli ambaye ataweza kumpa penzi ya dhati.

0 comments:

Chapisha Maoni