Jumanne, Septemba 02, 2014

MTOTO WA MIAKA 8 AGONGWA NA GARI NA KUFARIKI PAPO HAPO MBEYA

Mtoto mmoja ambaye hajatambuliwa jina, anaye kadiriwa kuwa na umri wa miaka7-9 amefariki dunia baada ya kugongwa na gari huko Sogea mkoani Mbeya.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na moja jioni huko Sogea Tunduma kata na tarafa ya Tunduma wilaya ya Momba mkoani Mbeya ambapo amemtaja dereva aliyesababisha kutokea kwa tukio hilo kuwa ni Keffa Mahenge mwenye umri wa miaka 29 aliyekuwa anaendesha gari lenye namba za usajili T 916 APD aina ya TOYOTA SURF HILUX. 
Hata hivyo chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika na wanaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo. 
Pamoja na hayo Msangi amewataka madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ili waweze kuepukana n ajali zinazo weza kuepukika.

0 comments:

Chapisha Maoni