Jumatatu, Agosti 18, 2014

KATI YA SHULE KONGWE TANZANIA, HII IKO TUKUYU-MBEYA, INAMIAKA 95

Vyumba vitatu vilivyokuwa vimejengwa na serikali ya mkoloni.
Shule hii inaitwa shule ya msingi tukuyu, inapatikana halmashauri ya wilaya ya Rungwe katika mji wa Tukuyu. ilijengwa na serikali ya wakoloni mnamo mwaka 1919, ni shule ya pili baada ya ile iliyoko amani mkoani Tanga, walimu wakuu waliowahi kuitumikia shule hii ni pamoja na Mlm M. Mwakibinga 1976-1979, Mlm Mbonde 1980-1981, Mlm Mwamundela 1981-1984, Mlm Tm Mwakasege 1984-1990, Mlm M andrew 1991-1993, Mlm N Madaraka 1993-1994 , Mlm Mashaka 1994-2005, Mlm Kasala 2005-2005 alikaa muda wa takribani miezi miwili, Mlm Kilembe Isaack 2005 mpaka sasa.
Majengo ya vyoo vya wasichana.
Majengo yaliyojengwa na serikali ya kikoloni ni vyumba viwili vya kusomea na chumba kimoja kilichokuwa ofisi pamoja na vyoo vyenye matundu 26 ya wanawake 13 na wavulana 13, cha ajabu alichosema mkuu wa shule ni kwamba vyoo havijawahi kujaa hata siku moja.
 Kibao cha shule kinachoonesha mwaka wa kujengwa shule 1919.

0 comments:

Chapisha Maoni