Mabingwa wa EPL Manchester City wanafikiria kumchukua kiungo wa Everton
Ross Barkley kwa pauni milioni 25 (Daily Mirror), boss wa West Ham Sam
Allardyce anafikiria kupanda dau kumchukua mshambuliaji wa kimataifa wa
Ecuador Enner Valencia aliyepachika mabao matatu katika Kombe la Dunia
(Daily Star), Liverpool wanataka kumchukua beki wa Seattle Sounders,
DeAndre Yedlin, na huenda wakamualika kwa majaribio katika mechi za
kabla ya kuanza msimu (Metro), Barcelona
bado hawajafikia makubaliano na Liverpool kuhusiana na uhamisho wa Luis
Suarez, mkataba huo hautarajiwi sasa kuafikiwa hadi wiki ijayo
(Guardian), beki wa zamani wa Chelsea Ashley Cole anafanya mazungumzo na
klabu ya Roma ya Italia kusaini mkataba wa miaka miwili (Daily Mail),
Tottenham na Arsenal zote zinamfuatilia beki wa kati wa Uholanzi Joel
Veltman (Daily Mirror), mshambuliaji wa Uholanzi Klaas-Jan Huntelaar
amesema atazungumza na Schalke kwanza baada ya kuhusishwa na klabu ya
Liverpool (Evening Standard), beki mwingine wa Uholanzi Daryl Janmaat
ananyatiwa na Newcastle na Manchester United (Daily Mail), kiungo
Mfaransa anayechezea Southampton, Morgan Schneiderlin ana uhakika wa
kuondoka na amewaambia wenzake kuwa hatorejea baada ya Kombe la Dunia
(Daily Star), QPR wanafikiria kumchukua mshambuliaji wa zamani wa
Arsenal, Eduardo (Daily Star), Chelsea wamefanya jaribio la kumsajili
kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos, ambaye pia anasakwa na Real Madrid
(Daily Star), meneja wa Arsenal, Arsene Wenger atamtoa Joel Campbell kwa
mkopo kwa msimu ujao. West Ham, Everton, Southampton na Newcastle zote
zinamtaka (Daily Mail), Alexis Sanchez amekatisha likizo yake ili
kutatua hatma yake Barcelona. Juventus na Arsenal wamewasilisha maombi
yao. Arsene Wenger ametoa dau la kuvutia zaidi (AS), Arsenal na
Southampton zote zinamuwanja beki wa kushoto wa Colombia Pablo Armero
(ESPN), Chelsea wametoa pauni milioni 11.8 kumsajili beki wa kushoto wa
Atlètico Madrid, Filipe Luis, lakini klabu hiyo inataka milioni
19(Marca). Share tetesi na wapenda soka.
0 comments:
Chapisha Maoni