Ijumaa, Juni 27, 2014

ZITTO NA KAFULILA WATUKANWA TENA KUWA NI TUMBILI NA WASHENZI, VIDEO IKO HAPA

SAKATA linalohusu kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), limechukua sura mpya baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kuwashambulia kwa maneno makali, wabunge wawili Zitto Kabwe wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) na David Kafulila wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi).
Fichuo ilikuwapo wakati Maswi akitumia maneno makali kwa kuyarudia, akikejeli nyaraka zinazotajwa kuwa ni ushahidi wa jinsi IPTL ilivyouza hisa zake na fedha kutolewa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika akaunti maalumu ya pamoja (Escrow), akisema nyaraka hizo ni karatasi za kufungia vitumbua zinazosambazwa na wabunge hao aliowaita “washenzi”.

Kauli hiyo ya Maswi imekuja siku mbili tu baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema kushambuliana na Kafulila kwa maneno makali malumbano yao yakianzia ndani ya Bunge na kuendelea walipotoka, kila mmoja akiamini kauli aliyoitoa ilikuwa ni sahihi.
Werema alimfananisha Kafulila na tumbili na yeye kumuita mwanasheria huyo mwizi. Tumbili ni mnyama wa porini wakati mwizi ni mtu anayetenda uhalifu kwa kuchukua kitu au mali isiyo yako. 
Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wake Dar es Salaam jana Ijumaa Juni 27, 2014, Maswi anasema;
Juzi AG alisema tatizo la nchi hii ni wanafiki na waongo… naungana nae kuwaita tumbili. Kama kuna mwanaume aje asema barabarani hayo maneno yake nimshughulikie. Wanajionyesha wanaume kumbe washenzi tu. Mimi sichukui rushwa najiamini.
Anakuja mshenzi mmoja anasema bungeni, kwanini asije huku barabarani akanitambua mimi nani. Werema alisema tumbili na mimi nasema tumbili…. Watu wanalilia hela za IPTL tu.
… Mwambie Kafulila nimesema wazi yeye ni mshenzi. Kafulila na mwenzake wamechukua hela na wamepewa hayo makaratasi na Mkono (Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono) wanafikiri sijui? Najua.. kwa sababu ya njaa njaa zao. Na nimemwambia kama mwanaume asema openly (wazi) hapa atantambua mimi nani.. Kwanini uende kusema bungeni na vipepeushi tu? Tusisemee kule ambapo tunajua ana kinga.
Sakata la IPTL ambalo linaendelea kuchafua hali ya hewa na kuzidi kuibua hasira za watendaji serikalini lilianza muda mtefu katikavyombo  vya habari.

0 comments:

Chapisha Maoni