Jumanne, Juni 10, 2014

WABUNGE WA TANZANIA EAC WAGUNDUA UCHAFU WANAOFANYIWA KATIKA BUNGE LA EAC

WABUNGE saba wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania, wamejiondoa kwenye jaribio la kutaka kumuondoa madarakani Spika wa Bunge hilo, Margareth Zziwa, baada ya kubaini kulikuwa na mchezo mchafu nyuma yake.
Walisema kuwa hoja hiyo haina maslahi ya Tanzania na iko kinyume na malengo ya ushirikiano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, wabunge hao wakiongozwa na Mwenyekiti wao Adam Kimbisa, Katibu wao, Shy-Rose Bhanji na Mwanasheria, Twaha Taslima, walisema masilahi ya Tanzania ndiyo kipaumbele kwao.

0 comments:

Chapisha Maoni