Jumanne, Juni 24, 2014

NIMEIPENDA HII 'NAMNA YA KUPATA KITU KILICHOIBIWA AU KUPOTEA'

Katika nyota na elimu ya Nambari (Numerology) kuna njia ya kuweza kukufanya uweze kugundua kilichoibiwa au kupotea au ambacho umekiweka mahala na huwezi kukumbuka ni wapi.

Njia ya kufanya ni kama ifuatavyo:

1. Unapopoteza kitu unatakiwa kwanza utulie usipate hofu wala kubabaika.

2. Unatakiwa utulize mawazo yako na uanze kukifikiria hicho ulichokipoteza.

3. Unatakiwa uandike kwenye karatasi nambari tatu kati ya 1-9 ambazo zitakuja katika akili yako kwa wakati huo.

4. Jumlisha namba hizo upate nambari moja.

Mfano: umeandika namba 4, 5, 2 unajumlisha 4 +5 + 2 = 11 unaendelea

1 + 1 = 2.

Majibu ni kama ifuatavyo:

KAMA IKIBAKI 1:

• Kitu hicho kinaweza kupatikana upande wa Kusini hasa katika sehemu muhimu ya nyumba yako, Sebuleni au Chumbani.

• Kiko karibu na pazia nyeupe au shuka nyeupe au nguo nyeupe katika sehemu tulizozitaja.

• Kama hukioni kitu hicho muulize mtoto aliyepo ndani ya nyumba yako atakuonyesha.

KAMA IKIBAKI 2:

• Kitu hicho kinaweza kupatikana upande wa Kusini hasa karibu na Karo au Beseni au sehemu mnayotumia kwa kufua nguo.

• Kitu hicho utakipata kwa msaada wa Mtu hasa Mwanamke anayeishi hapo kwako.

• Angalia sana sehemu ya kwenye tanki la maji au sehemu maji yanapopita au karibu na nguo zilizofuliwa.

KAMA IKIBAKI 3:

• Kitu hicho kinaweza kupatikana upande wa Kaskazini ndani ya makaratasi au vitabu au makabrasha yako au ukumbini.

• Umekipoteza katika sehemu ambayo ulikuwa ukifanyia kazi au ofisini au karibu na boksi au magazeti

• Angalia ndani ya Boksi au kwenye kabati la vitabu au katika kitu ambacho kinajifunga mara mbili kama faili au muulize mtoto.

KAMA IKIBAKI 4:

• Kitu hicho unacho mwenyewe lakini umesahau.

• Kiko upande wa Kaskazini angalia kwenye Rafu (Shelf) utakikuta hapo

• Kama hukioni angalia kwenye kabati la nguo au sehemu unapoweka tai zako au mikanda.

KAMA IKIBAKI 5:

• Kitu hicho kinaweza kupatikana kwa urahisi upande wa Magharibi. Hasa sehemu unazoweka kofia vilemba au kitunga.

• Jaribu kutafuta sehemu unazoekea nguo.

• Kitu kiko katika shubaka au kwenye kitu msatili au sehemu unayowekea viatu.

KAMA IKIBAKI 6:

• Kitu hicho itakuwa vigumu kukipata, lakini angalia upande wa mwisho Mashariki au Magharibi, sehemu ambayo kuna viatu au malapa.

• Jaribu kuangalia kwenye kitanda au kwenye stendi ya vitu au kwenye rafu (Shelf).

• Kama hukioni muulize Mumeo au Mkeo, kitakuwa katika vitu vyako vya binafsi.

KAMA IKIBAKI 7:

• Kuna uwezekano usikipate kitu hicho lakini jaribu kuangalia upande wa Mashariki katika kitu cheupe kama ni nguo au shuka au karatasi jeupe kiangalie utakiona hapo.

• Kuna uwezekano wa kudanganywa au watu wako kukataa kukupa taarifa kuhusu kupotea kwa kitu chako.

KAMA IKIBAKI 8:

• Kitu hicho kinaweza kupatikana upande wa Kaskazini hasa katika sehemu tambarare au jaribu ndani ya kabati.

• Kiko karibu na sehemu unapoweka vitu vyako vya thamani kama fedha na dhahabu.

• Ukianza kukitafuta angalia chini ya mguu wako utakiona.

KAMA IKIBAKI 9:

• Kitu hicho kinaweza kupatikana upande wa Mashariki hasa katika sehemu ambayo kuna nguo za watoto.

• Tia mkono wako kwenye nguo na papasa papasa utakiona.

• Kitu kilichopotea kiko ndani ya familia, Kama hukioni kiangalie kwenye chumba cha watoto au kwenye vitu vya zamani au kwenye sehemu yenye giza au kwenye kona.

0 comments:

Chapisha Maoni