Jumanne, Juni 24, 2014

ALIYETOKA JELA KWA MSAMAHA WA RAIS AUA TENA KWA KUNYONGA

Mtu mmoja anayedhaniwa kuwa ni jambazi anatafutwa na jeshi la polisi kwa madai ya kufanya matukio mbalimbali ya kiharifu likiwemo tukio la hivi karibu kumnyonga hadi kufa dada mmoja aliyetajwa kwa jina la Bahati Husein mkazi wa Ulongoni A Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Akizungunza na wanahabari, dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Moshi Hussein alisema mtu huyo ambaye anatambulika kwa jina moja la Godfrey, kabla ya kumuua dada yake alikuwa akimtamkia mara kwa mara kwamba ipo siku atamuua.
Tulikuwa tunaona kama utani maana alikuwa akisema suala la kumuua mara kwa mara na siku chache kabla ya kumuua walikuwa na ugomvi ambapo Godfrey alikuwa akimhisi dada yangu (ambaye kwa sasa ni marehemu) anamahusiana na mwanaume mwingine hali iliyosababisha kaka aje na kuwasuruhisha
anaeleza Moshi huku akilia kwa uchungu.
Aliendelea kusema baada ya kusuruhishwa alionekana kuridhika na kumtaka mkewe (marehemu) ampikie ugali ambapo marehemu alifanya kama alivyoagizwa lakini usiku wake akambyonga hadi kufa.
Baada ya kumuua aliondoka usiku huo huo na asubuhi alipiga simu kwa ndugu akisema eti anataka kuongea na mkewe kwa hiyo mtu aende ampe simu ili wazungumze wakati anajua nini amekifanya!
anasimulia Moshi.
Alipoulizwa wao walijuaje kama marehemu alinyongwa hadi kufa, Moshi alisema baada ya kifo hicho walikwenda kuripoti kituo cha polisi Stakishali ambapo kabla ya kujua kama ndugu yao ni marehemu walimchukuwa na kumkimbiza katika Hospitali ya Amana ambapo mara baada ya madaktari kumchukuwa vipimo iligundulika kuwa dada tayari alikuwa mfu.
Tulipohoji chanzo cha kifo chake ndipo tulipoambiwa kwamba vipimo vinaonyesha marehemu amenyongwa na shingo yake imevunjika mara mbili
alisema.
Aidha, akitoa historia ya mtu huyo anayetajwa kama jambazi sugu, kaka wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Husein, alisema kabla ya kutokea kwa tukio hilo Godfrey alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa kama hilo (la mauaji) na aliachiwa huru mwaka jana kwa msahama wa rais.
Hadi anakuja na kuishi na dada yetu bwana huyu alikuwa jela akitumika miaka 20 kwa kosa kama hili. Kwa sababu huyu jamaa (Godfrey) ni mtu mwenye wivu sana na chanzo cha kufungwa miaka 20 ilikuwa ni baada ya kumfumania mkewe na mwanaume mwingine gesti ambapo aliwauawa wote na kesi kwenda mahakamani na kukutwa na hatia na kufungwa miaka hiyo 20 leo kamuua dada yangu, ina niuma sana
alisema Abdallah.
Aidha, mjumbe wa eneo hilo la Ulongoni A ambaye jina lake hakulikuweza kupatikana mara moja alithibitisha kutokea tukio hilo.
Jitihada za kumpata Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi Ilala, Kamanda Mariathe Minangi hazikuzaa matunda baada ya simu yake kupokelewa na mtu aliyejitambulisha ni mlinzi wake na kudai RPC yupo kikaoni. Jitihada za kumtafuta RPC bado zingaliendelea kwa ajili ya kutolea ufafanuzi tukuio hili.

0 comments:

Chapisha Maoni