Mdada mmoja alitaka kujua kiasi gani anapendwa na mume wake, hivyo akataka kujua mumewe atafanya nini endapo ataamua kuondoka na kumuacha! Mwanamke huyo akaamua kuandika barua inayosema
Samahani mume wangu, nimeamua kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya mbali na wewe
Barua ile akaiweka juu ya meza iliyokuwa chumbani.
Baadaye jioni, muda wa Mumewe kurudi mwanamke huyo akajificha chini ya uvungu nwa kitanda mle chumbani Mume alipoingia chumbani akakuta ile barua juu ya meza, akaisoma kisha, akaandika maneno fulani kwenye ile ile barua, halafu akaanza kuimbaimba kwa furaha huku akipiga miluzi na akiwa anavua nguo.Akapiga simu na akasikika akisema hivi

hello mpenzi, nina raha sana leo.. yule mwanamke nuksi amesarenda mwenyewe kaondoka na kutuachia uwanja, jiandae nakuja
Muda huo huo Mume akaondoka.Mwanamke alipokuwa uvunguni akawa anatoka lakini amenyong'onyea na amelowa mashavu kwa machozi. Akasogea pale ilipo barua na akataka kujua mumewe aliandika kitu gani kwenye ile barua. Akakuta maneno haya
Nimeona miguu yako uvunguni, tafadhali andaa chakula nina njaa sana mumeo, ila nimetoka kidogo nafuata maziwa nilisahau kupitia. Nakupenda mke wangu

0 comments:
Chapisha Maoni